Wafanyakazi wa Clouds Media wapata ajali wakitoka kumzika Ruge
Habari zilizopo zinasema watu hao wamepata ajali wakiwa katika gari yao yenye namba za usajili T884 DNS ndani iliyokuwa na watu sita na wote wametoka salama.
Kupitia page yao ya instagram, Clouds TV imesema: Tunasikitika kuwataarifu kuwa sehemu ya timu yetu ya production (Watu 6) iliyokuwa ikitokea msibani Bukoba kurejea jijini Dar es Salaam imepata ajali ya gari maeneo ya nje kidogo ya Dodoma.
Tunamshukuru Mungu hakuna aliyepata madhara makubwa kutokana na ajali hiyo.
Tunamshukuru Mungu hakuna aliyepata madhara makubwa kutokana na ajali hiyo.
Tunatoa shukrani za dhati kwa mbunge wa jimbo la Dodoma mjini ndugu yetu Anthony Mavunde kwa msaada wa haraka aliowapatia vijana wetu ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu na vipimo zaidi Jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Clouds Media wapata ajali wakitoka kumzika Ruge
Reviewed by Zero Degree
on
3/06/2019 11:20:00 AM
Rating:
