Loading...

Bado tuko pamoja na Bocco, tunatambua mchango wake - Ahmed Ally


Uongozi wa Simba umebainisha kwamba utaendelea kusimama na nahodha wa msimu wa 2023/24 katika kikosi hicho John Bocco mshambuliaji bora wa muda wote Bongo.

Ipo wazi kwamba Bocco kwenye Ligi Kuu Bara anashikilia rekodi ya kufunga mabao zaidi ya 100 akiwa ni mzawa mwenye uwezo mkubwa kwenye eneo la ushambuliaji kwa miaka ya hivi karibuni.

Hatakuwa ndani ya kikosi cha Simba kwa msimu wa 2024/25 baada ya kukutana na Thank You akiwa ni mchezaji wa kwanza kuagwa rasmi na uongozi wa Simba.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wanatambua umuhimu wa wachezaji wao hivyo wataendelea kusimama nao kila wakati mpaka wao wenyewe waseme inatosha.

“Kawaida ya Simba ni kuhsehimu mchango wa wachezaji wake wote. John Bocco tunatambua mchango wake na tutasimama naye mpaka pale yeye mwenyewe akisema inatosha kwa kuwa ni familia yetu na atabaki kuwa kwenye familia.

“Unaona kuna mchezaji Mussa Mgosi yeye alicheza Simba na sasa anafundisha kwenye timu ya wanawake hata Suleiman Matola naye alicheza Simba kwa sasa anaifundisha Simba hivyo ni mwendelezo wetu kusimama na wachezaji wetu kila wakati.”
Bado tuko pamoja na Bocco, tunatambua mchango wake - Ahmed Ally Bado tuko pamoja na Bocco, tunatambua mchango wake - Ahmed Ally Reviewed by Zero Degree on 6/22/2024 08:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.