Dk Mwinyi afunga mjadala wanaotaka aongezewe muda
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi, amesema yeye ni muumini wa Katiba na sheria za nchi, hivyo wanaotoa maoni aongezewe muda wa miaka saba kukaa madarakani badala ya mitano wafunge mjadala huo.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zanzibar, Charles Hillary leo Jumatatu Juni 24, 2024, imesema maoni hayo yamekwenda mbali hata kutaka Uchaguzi Mkuu wa Rais usifanyike mwakani na kueleza kuwa jambo hilo halina tija wala faida kwa nchi na Chama cha Mapinduzi (CCM), chenye misingi ya kufuata demokrasia.
“Rais Dk Mwinyi ni muumini wa kufuata Katiba na sheria za nchi, tunapenda kusisitiza kwamba maoni haya si ya Mheshimiwa Rais wala sio ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.
“Kwa muktadha huu, Rais Dk Mwinyi ataendelea kuheshimu utaratibu uliowekwa wa Rais kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Aidha amewasihi wale wote wenye mawazo tofauti na hayo wafunge mjadala huo,” imesema taarifa hiyo.
“Kwa muktadha huu, Rais Dk Mwinyi ataendelea kuheshimu utaratibu uliowekwa wa Rais kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Aidha amewasihi wale wote wenye mawazo tofauti na hayo wafunge mjadala huo,” imesema taarifa hiyo.
Dk Mwinyi afunga mjadala wanaotaka aongezewe muda
Reviewed by Zero Degree
on
6/24/2024 07:30:00 AM
Rating: