Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 22 Juni, 2024

Leny Yoro, 18

Manchester United wamefanya mawasiliano ya awali na Lille kuhusu usajili wa beki wa Ufaransa Leny Yoro, 18.

Manchester United na Tottenham wanamtaka Jonathan David wa Lille, Wolves wakitaka pauni milioni 45 kwa ajili ya Max Kilman, huku Douglas Luiz anakaribia kuondoka Aston Vila.

Klabu ya Manchester United na Tottenham ni vilabu viwili kati ya vilabu vinavyomhitaji mchezaji wa Canada na mshambuliaji wa Lille Jonathan David, 24. (Sky Sports)

Klabu ya Wolves wanataka hadi £45m kwa Max Kilman kufuatia ofa ya West Ham ya £25m kwa mlinzi huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27. (Guardian)

Kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, anakaribia kuhama kutoka Aston Villa kwenda Juventus , huku Villa ikipokea winga Mwingereza Samuel Illing-Junior, 20, na kiungo wa kati wa Argentina Enzo Barrenechea, 23, pamoja na ada ya uhamisho ya £25m. (Mail)

Lazio wako tayari kumpa mlinda lango wa Ugiriki Christos Mandas, 22, pamoja na ada ya pauni milioni 15 katika jitihada zao za kumsajili mshambuliaji Muingereza Mason Greenwood, 22, kutoka Manchester United . (Il Messaggero)

Southampton wanapanga kumnunua winga wa Jamaica na Fulham Bobby De Cordova-Reid, 31, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu wa joto. (JSun)

Aaron Wan-Bissaka

Beki wa klabu ya Manchester United na England Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 26, anakaribia kuhamia Galatasaray na anatarajia kupewa mkataba wa miaka minne na timu hiyo ya Uturuki. (Bein Sports Turkey)

Kkabu za Chelsea na Bayern Munich zote zinaonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Mhispania Marc Guiu, 18, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 6m (£5.08m). (Fabrizio Romano)

West Ham na Nottingham Forest wamewasiliana na Arsenal kuhusu uwezekano wa kumnunua winga wa Uingereza Reiss Nelson, 24. (Football Insider)

Manchester United wana wasiwasi kwamba hawataweza kumnasa Rennes mwenye umri wa miaka 19, Desire Doue kwenda Old Trafford, huku klabu hiyo ya Ufaransa ikiweka bei ya juu inayomtaka kiungo huyo. (Givemesport)

West Ham na Brentford wameonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa zamani wa Everton Dominic Calvert-Lewin, 27. (FootballTransfers)

Roma wako tayari kufanya mazungumzo na Manchester City huku wakitafuta njia za kumnunua mlinzi wa Uhispania Sergio Gomez, 23. (Caughtoffside)

Klabu ya AC Milan wanavutiwa na kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28. (Corriere dello Sport)

Everton wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Senegal Illian Ndiaye, mwenye umri wa miaka 24, kutoka Marseille . (L'Equipe)

Xavi Simons, 21

Bayern Munich wako kwenye mazungumzo na Paris St-Germain kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Xavi Simons, mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports Germany)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 22 Juni, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 22 Juni, 2024 Reviewed by Zero Degree on 6/22/2024 10:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.