Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 23 Juni, 2024
Newcastle wanakaribia kumsajili Dominic Calvert-Lewin, Wolves wanakataa ofa ya Newcastle kwa Max Kilman, na Douglas Luiz anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Juventus.
Newcastle United wanakaribia kuinasa saini ya mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin, 27, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Everton. (Guardian)
Brighton wana nia ya kumsajili winga wa Uturuki Baris Alper Yilmaz, 24, kutoka Galatasaray.
Newcastle pia wametoa ofa ya fedha pamoja na mchezaji kwa beki wa kati wa Wolves Muingereza Max Kilman, 27. (Telegraph)
Everton wako kwenye mazungumzo na Newcastle kuhusu kumsajili winga wa Gambia Yankuba Minteh, 19.
Wolves tayari wamekataa ofa ya Kilman kutoka Newcastle ambayo pia iliuliza kuhusu kumsajili winga wa Ureno Pedro Neto, 24. (HITC)
Mchezaji wa Aston Villa Douglas Luiz anakaribia kuhamia Juventus na anatazamiwa kufanyiwa vipimo vya afya wiki ijayo nchini Marekani, ambapo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 yuko kwenye majukumu ya Copa America na Brazil. (Gianluca di Marzio)
Klabu za Manchester City na Manchester United zilichukua hatua za kuchelewa kumsajili Michael Olise, 22, ambaye anatarajiwa kujiunga na Bayern Munich, huku zote zikiangalia uwezekano wa kumruhusu winga huyo wa Ufaransa kusalia na Crystal Palace kwa mkopo kabla ya kujiunga nao msimu ujao. (Mirror)
Manchester United wako tayari kusubiri miezi tisa mingine kwa Dan Ashworth kuanza kazi kama mkurugenzi wao mpya wa michezo.
Mshambulizi wa Uingereza Marcus Rashford, 26 ameapa kurekebisha uhusiano wake uliovunjika na Erik ten Hag baada ya Manchester United kuthibitisha kuwa Mholanzi huyo atasalia kama meneja. (Sun)
Everton wanajiandaa kupokea ofa nyingine kutoka kwa Manchester United kwa ajili ya mlinzi wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21, baada ya hapo awali kukataa kandarasi iliyopunguzwa bei. (Mail)
Tottenham hawana nia ya kusalimu amri kwa Real Madrid au klabu nyingine yoyote inayotarajia kumsajili beki wa Argentina Cristian Romero, 26, msimu huu wa joto.
Jaribio la Leeds kutaka uhamisho wa Joe Rodon kutoka Tottenham kuwa wa kudumu linakaribia kuporomoka kwani kuna uwezekano mkubwa wa kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, huku Leicester, Ipswich na Southampton zikiwa na nia ya kumnunua beki huyo wa Wales, mwenye umri wa miaka 26.
Newcastle wamekataa nia ya awali kutoka kwa Liverpool kumsajili Minteh, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Feyenoord chini ya mkufunzi mpya wa klabu hiyo ya London Uingereza, Arne Slot. (Football Insider)
Aston Villa wameuliza kuhusu kupatikana kwa kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Brais Mendez, 27. (Express)
Juventus wanaweza kumpeana mshambuliaji wa Italia Federico Chiesa, 26, kama sehemu ya mpango unaowezekana wa kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 22. (La Gazzetta dello Sport)
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uholanzi Xavi Simons, 21 ameiambia Paris St-Germain kwamba anataka kuondoka msimu huu wa majira ya joto, huku Bayern Munich wakijaribu kupata mkataba wa mkopo na wajibu wa kumnunua, huku RB Leipzig wakitumai kumsajili tena mchezaji huyo ambaye alikuwa akihudumu kwa mkopo msimu uliopita. (Fabrizio Romano)
Beki wa Ujerumani Joshua Kimmich, 29 hana uwezekano wa kuongeza mkataba wake na Bayern Munich zaidi ya 2025 na klabu hiyo ya Ujerumani iko tayari kumuuza mchezaji huyo msimu huu wa joto. (Sky Sport Germany)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 23 Juni, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
6/23/2024 10:27:00 AM
Rating:
