Wizara ya madini isimamie sheria na kanuni za uchimbaji bora na salama - Dkt. Mpango
Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, ametoa maagizo saba yatakayosaidia kuboresha sekta ya madini nchini, ikiwemo wadau wote wa sekta hiyo kuzingatia, kufuata sheria na kanuni ikiwa ni pamoja na kutotorosha madini ili kuondoa usumbufu na kurahisisha utendaji wa shughuli zao.
Aidha, wachimbaji lazima wahakikishe wanakuwa mstari wa mbele kulipa tozo na ushuru halali ili kusaidia kuongeza mchango wa sekta ya madini katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.
Dk. Mpango alibainisha hayo juzi jijini Dodoma, wakati akifungua kongamano la wiki ya madini lililoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA).
”Wizara ya Madini zishirikisheni na Wizara mnazofanya nazo kazi katika eneo la uchimbaji madini kwa mfano wizara ya ardhi, maliasili na utalii, maji na mazingira kabla ya kutoa leseni kwa wachimba madini, ili kuepuka migogoro na muingiliano wa shughuli nyingine kulingana na matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo husika.
“Mfano hapa Dodoma hapo kwenye kilima cha UDOM eneo la Njedengwa, kuna uchimbaji wa madini ya kokoto unaendelea, hali ambayo inaharibu kabisa mazingira,” alisema Dk. Mpango.
Alisema mwaka juzi niliagiza kilima hicho chote kipandwe miti ili kupendezesha mandhari lakini kuna viongozi wametoa vibali kuchimba kokoto na kifusi.
“Waziri wa madini na waziri wa nchi muungano na mazingira angalieni namna bora ya kuratibu shughuli za uchimbaji madini, ili kuepuka uharibifu wa mazingira katikati ya miji na majiji,” alisema.
Alisema bado kuna wachimbaji wengi wadogo wanafanya shughuli za uchimbaji kwa kubahatisha na kutumia muda mwingi na nguvu kubwa na kuambulia kidogo na wakati mwingine kukosa kabisa.
Alisema kutokana na hali hiyo wizara ya madini lazima iongeze wigo na jitihada za utafiti wa madini kupitia taasisi ya GST, ili kuwaongoza vyema wachimbaji wetu wadogo kutoka kwenye kuchimba kwa kubahatisha.
Alisema serikali imekuwa ikipoteza nguvu kazi kubwa kutokana na vifo vinavyotokea katika migodi mbalimbali.
“Wizara ya madini isimamie sheria na kanuni za uchimbaji bora na salama, ili kuepuka ajali zisizo za lazima zinazopelekea vifo na majeraha kwa wachimbaji wadogo,” alisema.
Alisem ajira na mapato yanapotea kutokana na kutosimamia ipasavyo utaratibu wa kuongeza thamani madini yanayopatika nchini.
Aidha, aliitaka wizara ya madini kusimamia utekelezaji wa mkakati wa kuhakikisha madini yanayochimbwa yanaongezwa thamani nchini, jambo litakalosaidia upatikanaji wa mapato na ajira kwa Watanzania.
“Wizara na tume ya madini hakikisheni wachimbaji wadogo waliopata leseni za madini na kuwekeza mitaji yao wasinyang’anywe kwa kigezo kuwa walipewa leseni hizo kwenye maeneo ya wachimbaji wakubwa,” alisema.
Dk. Mpango alisema suala lisiloeleweka vizuri ni kumpatia mchimbaji mdogo leseni ya uchimbaji madini na baada ya kuanza uwekezaji ananyang’anywa na mamlaka ile ile iliyompatia.
Alisema hali hiyo inaleta hisia za uwezekano wa uwepo wa mazingira ya rushwa.
Vile vile, alitaka wizara hiyo na tume ya madini kuangalia uwezekano wa kuwataka wachimbaji wakubwa na wa kati wanaochimba madini yenye thamani kubwa kurejesha mchango wao kwa jamii katika maeneo yanayowazunguka.
“Kwa mfano hapa Dodoma katika vijiji vya Asanje, Duluu, Gawaye na Itiso kuna uchimbaji wa madini unaoendelea, lakini wananchi wa maeneo hayo hawanufaiki kabisa na chochote,” alisema.

Reviewed by Zero Degree
on
6/22/2024 12:35:00 PM
Rating: