Mwanafunzi ‘aiba’ basi ili asikose mtihani
Ingawa aliadhibiwa, yeye na wenzake walifika shuleni kwa wakati |
Ajabu ni kwamba, mwanafunzi huyo amesema hakuwahi kuendesha basi kabla ya kisa hicho.
Mwanafunzi mmoja wa shule ya upili Afrika Kusini aliiba basi na kulitumia kufika shuleni ili asikose mtihani wa somo la hesabu.
Mwanafunzi mmoja wa shule ya upili Afrika Kusini aliiba basi na kulitumia kufika shuleni ili asikose mtihani wa somo la hesabu.
"Hapana, ni gari tu la kawaida," Le-Aan Adonis ameambia wanahabari.
Mwanafunzi huyo wa umri wa miaka 21 pamoja na wenzake, waliachwa wamekwama kijijini mkoa wa Western Cape baada ya dereva wa basi aliyefaa kuwasafirisha umbali wa kilomita 30 kugoma na kutofika kazini.
Kijana huyo, baada ya kuona funguo za gari zilikuwa zimeachwa ndani ya basi, aliamua kulichukua, kuwa dereva na kuliendesha.
Lakini alisimamishwa na afisa wa trafiki na kupigwa faini ya $360 (£236) kwa kuendesha basi bila leseni na bila cheti cha kuendesha magari ya umma.
Alipoulizwa atalipaje faini hiyo, alijibu: “Wazazi wangu hawana pesa, hivyo iwapo kuna mtu anaweza kunisaidia kulipa faini hiyo, nitashukuru sana.”
Alijipata taabani, lakini kwa wanafunzi wenzake yeye ni shujaa kwani ilikuwa muhimu sana kwao kufanya mtihani huo wa kumaliza shule, na hawakuchelewa.
Source: BBC
Mwanafunzi ‘aiba’ basi ili asikose mtihani
Reviewed by Zero Degree
on
11/07/2015 04:02:00 PM
Rating: