MAPYA: Wema Sepetu amuingiza mkenge Diamond
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kipo karibu na Diamond, baada ya Wema kubanwa na wafanyakazi wa Tanesco na Dawasa akidaiwa kutumia huduma hizo ‘kimazabe’ na kwamba ni kwa miaka kadhaa, Diamond alishtuka kwani anavyojua yeye walikuwa wakitumia maji na umeme kwa malipo sahihi.
"Taarifa kwamba Wema alikuwa akitumia maji na umeme kwa muda mrefu bila kulipia imemshangaza sana Diamond. Anachosema ni kwamba, Wema kamuingiza mkenge kwani wakati wako pamoja (kimapenzi) alikuwa akitoa pesa kwa ajili ya kulipia huduma hizo.
“Hata hao wanaosema kwamba, Diamond aliujua mchezo huo wanamuonea maana alikuwa akitoa mkwanja kwa ajili ya chakula, maji na hata umeme. Sasa kusikia kwamba wakati anaishi pale na Wema huduma hizo hazikuwa zikilipwa ameshangaa sana,” alisema rafiki huyo wa Diamond na kuongeza:
“Hata hivyo, Diamond mwenyewe hataki kuongelea suala hilo kwa kuwa uhusiano wao ulishaisha licha ya kwamba anasisitiza kuwa, kama kweli halipii umeme na maji tangu enzi za penzi lao, kamuingiza mkenge kupitiliza.” Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Wema kwa njia ya simu ili kujua kama kweli deni analodaiwa la maji na umeme ni la tangu akiwa na Diamond, lakini simu yake haikuweza kupatikana hewani.
Alipotafutwa Diamond kuzungumzia sakata hilo alisema kuwa, yeye na Wema walishaachana hivyo kuanza kumzungumzia haiwezi kuleta picha nzuri. “Nikiwa pale kwa Wema nilikuwa kama mshua, nilikuwa natoa mkwanja kwa ajili ya matumizi ya msosi, maji na hata umeme sasa kama yametokea hayo kwamba alikuwa akitumia huduma hizo bure, mimi siwezi kuongelea hayo,” alisema Diamond.
Wiki mbili zilizopita, Wema alikwaa msala wa kudaiwa kutumia umeme kwa kuchezesha mita. Kikosi kazi toka Tanesco, kilivamia nyumbani kwake, Makumbusho na kukata umeme ikidaiwa anadaiwa pesa nyingi ambazo hazikuwekwa wazi. Siku tatu mbele, jamaa wa Dawasa nao walimfanyia ‘ziara’ ya kushtukiza na kumkuta na kosa la kutumia maji huku akiwa amegeuza mita hali inayomwingiza katika wateja wanaoonekana kuibia taasisi hiyo. Wakasema deni analodaiwa mlimbwende huyo ni shilingi milioni tisa (9,000,000).
Source: GPL
MAPYA: Wema Sepetu amuingiza mkenge Diamond
Reviewed by Zero Degree
on
12/18/2015 11:01:00 AM
Rating: