Loading...

Hii hapa kauli ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe baada ya Rais kutengua uteuzi wa waziri wa mambo ya ndani.


Saa chache baada ya Rais Magufuli kutangaza kumfuta kazi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga kutokana na kuingia bungeni akiwa amelewa Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameamua kutoa maoni yake juu ya maamuzi aliyofanywa na Rais Magufuli.

Akasema “Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja – hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu kwa kiongozi wa aina yake. Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi ‘ no nonsense”.

Hivi karibuni Zitto alinukuliwa na Vyombo mbalimbali vya Habari akisema Kitwanga si ‘size’ yake na kuwataka wananchi wampuuze kwa madai ya kuwatumia vijana wa (UVCCM) kueneza propaganda kwamba Zitto anaihujumu serikali ya Magufuli.

Mbali na hayo pia wabunge wa upinzani waliungana kumshinikiza Rais Magufuli amtumbue Kitwanga baada ya kubainika kuwa mmoja kati ya wamiliki wa Kampuni ya INFOSYS iliyotumika kufunga mashine za kuchukua alama za vidole (AFIS) katika Vituo vya Jeshi la Polisi Nchini kwa gharama ya Sh 37 bilioni ambapo hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 pekee vya polisi ambapo tayari kampuni hiyo imelipwa Sh. 34 bilioni ikiwa ni asilimia 99 ya fedha hizo.





ZeroDegree.
Hii hapa kauli ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe baada ya Rais kutengua uteuzi wa waziri wa mambo ya ndani. Hii hapa kauli ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe baada ya Rais kutengua uteuzi wa waziri wa mambo ya ndani. Reviewed by Zero Degree on 5/21/2016 09:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.