Loading...

Mkongwe Diego Maradona apata kazi hii katika Shirikisho la soka Duniani [FIFA]

ZURICH (AP) Diego Maradona anapata nafasi ya kuwa balozi wa FIFA. Uongozi unataka kuhakikisha kuwa mkongwe huyo wa Argentina "ana jukumu kubwa katika shughuli za FIFA kukuza mchezo wa soka duniani kote," ikiwa ni pamoja na timu yake ya mashujaa.

FIFA wanasema Maradona, mwenye umri wa miaka 56 atashiriki katika "miradi husika ya maendeleo."

Maradona alitangaza jukumu lake jipya siku ya Alhamisi wiki hii, na kusema FIFA imekuwa "safi na yenye uwazi" chini ya uongozi wa Rais Gianni Infantino.

Maradona alikuwa katika 'bifu' na Rais wa zamani wa FIFA, Sepp Blatter na kiongozi wa muda mrefu wa soka nchini Argentina, Julio Grondona aliyekuwa makamu wa rais mwandamizi 
FIFA ambaye alifariki dunia mwaka 2014.

Mwezi uliopita, Maradona alicheza mpira katika makao makuu ya FIFA wakati wa ziara yake ya kwanza tangu Novemba mwaka 2009, alopofika wakati wa kesi yake ya kinidhamu. Kocha huyo
 wa zamani wa Argentina, alitemwa baada ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.
Mkongwe Diego Maradona apata kazi hii katika Shirikisho la soka Duniani [FIFA] Mkongwe Diego Maradona apata kazi hii katika Shirikisho la soka Duniani [FIFA] Reviewed by Zero Degree on 2/11/2017 04:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.