Loading...

FIFA yaifungia nchi ya Mali kushiriki michuano ya kimataifa kwa madai ya serikali kuingilia soka

Fifa imetangaza kuifungia nchi ya Mali kushiriki michuano ya kimataifa kwa madai ya serikali kuingilia masuala ya soka.

Waziri wa Michezo wa Mali, Housseini Amion Guindo aliamua kuunda kamati ya muda kuendesha Shirikisho la Soka la Mali (Femafoot) baada ya kuona uongozi uliokuwa madarakani kutokuwa sahihi.

Lakini baada ya Femafoot kufikisha malalamiko yake Fifa, shirikisho hilo la soka la limataifa, likaiamuru serikali ya Mali, kuvunja kamati hiyo hadi Ijumaa.

Hii ndio baraua ya FIFA kwenda kwa Mali



Baada ya kuona hakukuwa na utekelezaji hadi leo usiku huku zikiwa zimebaki saw chache kabla ya muda kufika, Fifa imetangaza kuifungia Mali.
FIFA yaifungia nchi ya Mali kushiriki michuano ya kimataifa kwa madai ya serikali kuingilia soka FIFA yaifungia nchi ya Mali kushiriki michuano ya kimataifa kwa madai ya serikali kuingilia soka Reviewed by Zero Degree on 3/18/2017 11:18:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.