Loading...

Himid Mao na Jonas Mkude wapewa unahodha Stars

Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga amemtangaza Mbwana Samatta kuendelea kuwa nahodha wa timu hiyo lakini amefanya mabadiliko kwa wasaidizi wa Samatta.

Afisa habari wa TFF Bw. Alfred Lucas amesema, Himid Mao na Jobas Mkude watakuwa wasaidizi wa Mbwana Samatta ambaye ndio nahodha mkuu wa Stars. Himid na Mkude watavaa kitambaa cha unahodha wakati wa mechi zinazohusu mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Himid Mao
Inapotokea Stars inacheza muchuano ya FIFA au AFCON nahodha anabaki kuwa Mbwana Samatta lakini ikitokea inacheza michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) manahodha watakuwa ni Himid Mao na Jonas Mkude wakisaidiana kwa pamoja,” amesema Lucas.

Jonas Mkude, Simba SC
Himid na Mkude ni wasaidizi wapya wa Samatta wakichukua nafasi ya John Bocco ‘ Adebayor’ ambaye hajaitwa kwenye kikosi cha Stars chini ya Salum Mayanga.
Himid Mao na Jonas Mkude wapewa unahodha Stars Himid Mao na Jonas Mkude wapewa unahodha Stars Reviewed by Zero Degree on 3/21/2017 05:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.