Loading...

Hizi hapa timu ambazo hazijafungwa katika uwanja wa nyumbani msimu huu

Ukiacha Juventus ambaye hadi sasa katika michezo 33 hakuna mechi waliyopigwa, kuna timu ambazo msimu huu hawajapoteza mchezo hata mmoja wa ligi katika uwanja wao wa nyumbani.

Tottenham Hotspur.

Katika msimu huu wa ligi hadi sasa Tottenham wameshacheza michezo 14 katika uwanja wao wa nyumbani wa White Hart Lane. Hakuna timu ambayo imetembelea uwanja huo na kuondoka na alama zote 3, Hart Lane pamekuwa pagumu sana kwa wapinzani kwani kati ya mechi hizo 14 walizocheza wameshinda michezo 12 na kutoka suluhu miwili. Tottenham kwa ujumla msimu huu wamefunga magoli 33 na kufungwa 7 tu, wanatafuta ubingwa wao wa kwanza tangia mwaka 1961.

Real Madrid.

Madrid msimu huu pamoja na kwamba kuna kipindi walikuwa wakipatwa na matokeo yasiyoeleweka lakini nao hawajawahi kifungwa nyumbani. Katika ligi yao ya nyumbani Real Madrid msimu huu wamepoteza michezo miwili tu dhidi ya majirani zao Athletico na ule dhidi ya Sevilla. Lakini hawajawahi kufungwa wakiwa Santiago Bernabeu kwani michezo yao 14 waliyocheza uwanjani hapo wameshinda michezo 11 na kusulu michezo mitatu, na wakiwa wamefunga magoli 36.

Juventus.

Uwanja wa nyumbani wa Juventus umekuwa kama Jehannam kwa timu zinazoenda kupatembelea msimu huu. Katika ligi ya Italia hakuna timu ambayo imeambulia alama hata moja katika uwanja huo. Juventus wamechukua alama zote 45 katika michezo 15 waliyocheza uwanjani hapo, na ni kati ya viwanja vigumu sana kucheza dhidi yao. Si hivyo tu bali katika michezo 33 kwa ujumla ya Juventus hawajapoteza mchezo hata mmoja.

Bayern Munich.

Allianz Arena napo ni pagumu, uwanja huo wa nyumbani wa Bayern Munich hawajawahi kuangusha alama 3 katika uwanja huo. Hadi sasa katika ligi yao ya nyumbani Bayer Munich wameshacheza michezo 12 katika uwanja huo, kati ya michezo hiyo wameshinda mara 9 huku wakitoka sare mara 3 na kupata jumla ya magoli 38.Fc Koln,Hoffeinheim na Schalke 04 ndio timu pekee zilizogawana alama na Bayern katika uwanja huo.

Borussia Dortmund.

Wapinzani wakubwa wa Bayern Munich katika ligi ya Ujerumani, Dortmund nao wakiwa Westfalenstadion hawajapoteza mchezo hata mmoja. Wameshacheza michezo 11 uwanjani hapo na katika michezo hiyo wameshinda mara 8 huku wakitoka suluhu mara tatu na kufunga jumla ya magoli 28.

PSG.

Miamba ya Ufaransa, wakiwa nyumbani kwao wameshinda kwa wastani wa 64% na zilizobaki wametoa suluhu. Michezo 14 waliyocheza wamepata suluhu michezo 5 huku wakishinda michezo 9 kwa idadi ya magoli 28, wakiwa nyumbani kwao wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara 5 tu.
Hizi hapa timu ambazo hazijafungwa katika uwanja wa nyumbani msimu huu Hizi hapa timu ambazo hazijafungwa katika uwanja wa nyumbani msimu huu Reviewed by Zero Degree on 3/18/2017 04:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.