Loading...

Willy Caballero amefaulu vipimo vya afya Chelsea, imeripotiwa!


Golikipa Willy Caballero yuko kwenye hatua za mwisho kuitwa mchezaji wa Chelsea baada ya kufaulu vipimo vya afya katika klabu hiyo, kwa mujibu wa habari iliyotolewa na gazeti la 'The Times'.

Gazeti hilo linadai kwamba, Caballero amefaulu vipimo vya afya katika klabu hiyo na amekubaliana na vigezo na mashariti katika ofa yake aliyopewa.


Caballero ameakuwa chaguo la pili baada ya Joe Hart katika kikosi cha klabu ya Manchester City kabla hajapelekwa kwa mkopo kwenye Ligi ya Sirie A ya Italia mwaka jana.

Ripoti hiyo inasema kwamba, Golikipa huyo anaenda kuwa chaguo la pili Stamford Bridge msimu ujao nyuma ya Thibaut Courtois.

Hiyo inakuja baada ya ripoti kudai Caballero amekubaliana na vigezo na mashariti alivyopewa na Mabingwa wa Ligi Kuu na anaelekea kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Chelsea katika majira haya ya joto siku ya Tarehe 1, Julai.

Raia huyo wa Argentina atajiunga na Chelsea akiwa kama mchezaji huru kutokea Man City wakati mkataba wake utakapokuwa umemalizika mwishoni mwa mwezi huu pamoja na kwamba ametokea katika kikosi cha kwanza mara kwa mara msimu uliopita.

Willy Caballero amefaulu vipimo vya afya Chelsea, imeripotiwa! Willy Caballero amefaulu vipimo vya afya Chelsea, imeripotiwa! Reviewed by Zero Degree on 6/27/2017 01:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.