Loading...

Dortmund kutoiongezea Chelsea muda wa kupeleka ofa


Chelsea wanamatamanio makubwa ya kumnasa mshambuliaji hatari wa Borrusia Dortmund, lakini bado hawajapeleka ofa katika klabu hiyo.

'Future' Aubameyang inabakia kutofahamika na Chelsea ndio waliohusishwa naye kwa kiasi kikubwa, hata hivyo, wanaonekena kutuliza akili kwanza kwa kuto taka kurukia mambo kwa sababu fulani fulani.

Ukiachilia mbali tetesi zinazoendelea, CEO wa Dortmund, Watzke anasema hujakuwepo na ofa yoyote walikwisha pokea kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 na kwao dirisha la usajili liko linaelekea kufungwa.

Klabu zenye matumaini ya kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang zimebakiwa na siku chache kuanzisha mazungumzo na Borussia Dortmund, anasema Hans-Joachim Watzke.


“Hatujapokea ofa yoyote,,” aliliambia gazeti la 'Welt am Sonntag' la nchini Ujerumani.

“Tutasubilia kwa muda wa siku chache zaidi lakini sio kusubiri sana tena. Binafsi ningependelea endapo angesalia klabuni.

“Lakini kuna klabu kadhaa ndani ya sayari hii ambapo anaweza kujipatika kipato kikubwa zaidi ya hapa.”
Dortmund kutoiongezea Chelsea muda wa kupeleka ofa Dortmund kutoiongezea Chelsea muda wa kupeleka ofa Reviewed by Zero Degree on 7/16/2017 07:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.