Loading...

Timoue Bakayoko atambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Chelsea


Chelsea wamekamilisha taratibu za uhamisho wa Bakayoko. Mashabiki wa 'The Blues' sasa wameshusha pumzi baada ya Bakayoko rasmi kusaini mkataba na Chelsea.


Chelsea sasa wamefanikiwa kusajili mchezaji wa tatu katika majira haya ya joto baada ya kumnunua Timoue Bakayoko kutoka Monaco.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano na Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa kiasi cha pesa ambacho mpaka sasa ni makadirio tu, lakini kiwango kamili cha malipo yaliyofanywa bado hakijawekwa wazi.

Bakayoko ameisaidia Monaco kushinda Taji la Ligue 1 ya Ufaransa msimu ulioisha na vile vile, akaisaidia timu yake kufika nusus fainali ya Ligi ya Mabingwa (UEFA).

Raia huyo wa Ufaransa atakua sasa atakua na matazamio makubwa kuelekea mchezo wake wa kwanza na timu yake kama inavyotarajiwa ifikapo Agosti 
12 wakati Chelsea watakapoikaribisha Bunley Stamford Bridge.

Kiungo huyo wa Monaco, Timoue Bakayoko pia amethibitishwa kuhamia Stamford Bridge, na hatimaye klabu kutangaza dili hilo rasmi.

Wabrazili wawili, Luiz na Willian walitoa vionjo vya mwanzo kuhusiana na usajili huo pale walipopiga picha ya pamoja wakiwa Bakayoko London.

Bakayoko alikuwa Cpbham kukamilisha vipimo vya afya siku ya Ijumaa kabla ya kutolewa kwa taarifa ya kwamba tayari amesaini mkataba na Chelsea, na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Uingereza watatakiwa kulipa kiasi kinachokadiliwa kuanzia paundi milioni 40 na zaidi kwa ajili ya kiungo huyo mwenye miaka 22.


Pia kuvuja kwa picha iliyomwonyesa Bakayoko akiwa katika mazungumzo na Conte katika mazoezi baada ya kusaini mkataba na klabu hiyo.
Timoue Bakayoko atambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Chelsea Timoue Bakayoko atambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Chelsea Reviewed by Zero Degree on 7/16/2017 02:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.