Loading...

Ndege ya kijeshi ya Marekani yaanguka katika pwani ya Australia


Operesheni ya uokoaji inafanyika baada ya ndege ya kijeshi ya Marekani kupotea katika pwani ya Australia.

Kisa hicho kilichoshirikisha ndege aina ya MV-22 Osprey inayomilikiwa na wanamaji wa Marekani inatoka eneo la Okinawa nchini Japan.

Kitengo cha wanamaji cha tatu kilisema kuwa ndege hiyo ilipaa kwa opresheni za kawaida kabla ya kuingia majini.

Makundi ya waokoaji yaliwanusuru watu 23 lakini maafisa wengine 3 hawajapatikana.

Vyombo vya habari vya Australia vimeripoti kwamba kisa hicho kilitokea wakati wa jaribio kutua katika meli ya kubeba ndege.

MV 22 Osprey inaweza kubeba watu 24 mbali na wafanyikazi 4.

Iko sawa na ndege ya kawaida lakini ina mbawa kama yale ya helikopta ambayo huisaidia kupaa wima.

Gazeti la la telegraph nchini Australia ilinikuu duru za kijeshi ambazo zinasema kuwa kisa hicho kilitokea wakati ndege hiyo ilipokuwa ikijaribu kutua katika meli ya kubeba ndege za kijeshi ya USS Ronald Reagan
Ndege ya kijeshi ya Marekani yaanguka katika pwani ya Australia Ndege ya kijeshi ya Marekani yaanguka katika pwani ya Australia Reviewed by Zero Degree on 8/05/2017 08:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.