Loading...

Ujumbe wa Torres kwa Chelsea baada ya kupangwa kundini na Atletico Madrid Ligi ya Mabingwa


Torres alipost ujumbe mfupi kwenye Instagram kwa Chelsea baada ya droo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Timu ambazo Chelsea itakabiliana nazo kwenye hatua ya makundi tayari zimeshatangazwa rasmi.

Chelsea wamepangwa kundi moja na Atletico Madrid, Roma na Qarabag kwenye Kundi C la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA).

Baada ya kushindwa kufuzu kushiriki UEFA msimu uliopita, vijana hao wa Antonio Conte watakuwa na matamanio makubwa ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu ili kumaliza katika nafasi nzuri.

Baada ya droo kutangazwa, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Fernando Torres aliandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Twitter na Instagram.


“Narudi Stamfordbridge kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa,” aliandika Torres, pamoja na kuweka picha zikimwonyesha akisherehekea kufunga goli akiwa Atletico na ya wakati alipokuwa Chelsea. “Nina furaha kubwa sana kuiona Chelsea imerejea kwenye mashindano. Tutaonana hivi karibuni@chelseafc “.

Akiwa kipenzi cha baadhi ya mashabiki, Torres anaweza kutegemea ukaribisho wa heshima wakati atakaporudi StamfordBridge tarehe 5 Desemba.

A post shared by 🅵🅴🆁🅽🅰🅽🅳🅾 🆃🅾🆁🆁🅴🆂 (@fernandotorres) on
Ujumbe wa Torres kwa Chelsea baada ya kupangwa kundini na Atletico Madrid Ligi ya Mabingwa Ujumbe wa Torres kwa Chelsea baada ya kupangwa kundini na Atletico Madrid Ligi ya Mabingwa Reviewed by Zero Degree on 8/27/2017 10:11:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.