Loading...

Ujumbe wa Thiery Henry kwa Conte kuhusu Bakayoko


Thiery Henry anafikiri kwamba, Timoue bakayoko angetakiwa kuanza kwenye mechi ya Chelsea dhidi ya Arsenal Jumapili iliyopita.

Thierry Henry amemwambia meneja wa Chelsea kwamba alifanya kosa kubwa kutomuanzisha Bakayoko kwenye mechi ya Chelsea na Arsenal  iliyomalizika kwa sare ya bila kufungana.

Conte alichagua kumuanzisha Cesc Fabregas na N’Golo Kante katika kiungo wakati wa mchezo dhidi ya vijana wa Arsene Wenger.

Bakayoko aliachwa benchi kabla ya kupewa nafasi kwenye kipindi cha pili cha mechi hiyo iliyochezewa Stamford Bridge.

Na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Henry anahisi kwamba Conte alifanya kosa kwa kutomuanzisha Bakayoko kwenye mchezo huo.

Akizungumza na 'Sky Sports' baada ya mechi hiyo, Henry alisema: “Nafikiri walikosea (Chelsea) kidogo.

“Tiemoue Bakayoko alitakiwa aanzishwe kipindi cha kwanza. Cesc Fabregas angecheza upande wa juu na Bakayoko angecheza karibu na N’Golo Kante.”
Ujumbe wa Thiery Henry kwa Conte kuhusu Bakayoko Ujumbe wa Thiery Henry kwa Conte kuhusu Bakayoko Reviewed by Zero Degree on 9/19/2017 07:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.