Loading...

Jibu la serikali kufuatia waraka wa Maaskofu


Wakati wa waraka uliotolewa na Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) mwishoni mwa wiki iliyopita umeendelea kuibua mjadala mkubwa nchini Tanzania.

Rais Magufuli amewaomba wahubiri na maaskofu wazungumzie ujenzi wa viwanda vya dawa nchini ili Tanzania isinunue dawa nje ya nchi.

Amesema hayo akiwa katika hafla fupi jijini Dar es salaam ya ugawaji wa magari ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini.

Katika waraka wa ujumbe wa pasaka uliosomwa jana katika makanisa ya Kilutheri kote nchini Tanzania na kusambaa katika mitandao ya kijamii, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo.
Utekwaji wa watu wa hivi karibuni, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi ni baadhi tu ya mambo yaliyotajwa katika waraka huo.


Serikali ya Tanzania kwa sasa imejibu kwa kusema kuwa sasa haioni cha kujibu na kwamba inawatakia tu waumini kheri ya Pasaka.

Lakini pia Watanzania wamekuwa na hisia tofauti kuhusu viongozi wa dini kuzungumzia hali ya kisiasa nchini humo.

Waraka huu unakuja mwezi mmoja baada ya ule wa maaskofu wa kanisa katoliki ambao nao ulionya juu ya kuminywa kwa haki ya kufanya shughuli za kisiasa kama mikutano ya hadhara na maandamano.

Wengi bado wanasubiri kuona waraka huu utakuwa na matokeo gani sasa na siku za usoni.
Jibu la serikali kufuatia waraka wa Maaskofu Jibu la serikali kufuatia waraka wa Maaskofu Reviewed by Zero Degree on 3/26/2018 07:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.