Loading...

Manchester United, Chelsea kushindania saini ya kiungo wa Arsenal


Arsenal inaweza kukabiliana na ushindani mkubwa kumbakisha kiungo wake kwenye majira ya joto.

Manchester United na Chelsea zinatarajiwa kushindania saini ya kiungo wa klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey. Kiungo huyo kutoka Wales amefanikwa kuziteka akili za mahasimu wakubwa wa Arsenal kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Chelsea imekuwa ikimfuatilia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa lengo la kuendelea mkakati wao wa kuimarisha kikosi kwa kujaza wachezaji wenye uzoefu. Sasa Man United imeripotiwa kuingia kwenye mbio hizo kuwania saini ya Ramsey, ikidaiwa Jose Mourinho anavutiwa sana na kipaji chake na ana mpango wa kumuunganisha na Alexis Sanchez.

Aaron Ramsey
Ramsey anaweza kuwa sokoni kwa bei nafuu kwenye majira ya joto. Anakaribia kufikia miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake na hadi hivi sasa bado anakataa kusaini mkataba mpya Emirates.

Arsenal walijikuta katika hali kama hiyo kwa Sanchez na Oxlade-Chamberlain, ambao walikataa ofa za kuongeza mikataba yao na kuondoka kwenda United pamoja na Liverpool msimu huu.
Manchester United, Chelsea kushindania saini ya kiungo wa Arsenal Manchester United, Chelsea kushindania saini ya kiungo wa Arsenal Reviewed by Zero Degree on 3/22/2018 02:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.