Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 20 Machi, 2018

Beki wa klabu ya Chelsea, Marcos Alonso
Lionel Messi ameiambia timu ya usajili ya klabu ya Barcelona imsajili beki wa  Chelsea, Marcos Alonso badala ya David Alaba wa Bayern Munich.

Arsenal na Tottenham zimepewa na nafasi kubwa ya pekee baada ya klabu ya Bayern Munich kujitoa kwenye mbio za kuwania saini ya nyota wa Bordeaux na timu ya taifa ya Brazil, Malcom. (Express)

Lionel Messi amesema kuwa anaweza asipate nafasi nyingine tena kama timu yake ya taifa ya Argentina itashindwa kuchukua Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kwenye majira ya joto.

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesema kuwa angependela kucheza timu moja na Neymar. (ESPN)

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anafanya mpango wa kumnasa nyota wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon kwa pauni milioni 40, Luke Shaw akitarajiwa kuondoka old Traford.

Real Madrid, Paris Saint-Germain na Barcelona zote zinatazamia kuandika rekodi ya usajili kwa kumnasa winga wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah kwa pauni milioni 200.

Nick Pope
Burnley wako tayari kuongeza mara mbili ya mshahara anaolipwa golikipa wa Uingereza, Nick Pope kumfanya aachane na uhamisho kwenda Newcastle.

Luke Shaw hategemei kulazimishwa kundoka Manchester United na meneja wa klabu hiyo, Jose Mourinho kwenye majira ya joto.

Arsenal wanajiandaa kumsajili golikipa wa Bayer Leverkusen, Bernd Leno kwa pauni milioni 25.

Roberto Martinez anasema kuwa kamwe hatamtumia Eden Hazard kama mshambuliaji kivuli katika timu ya taifa ya Ubelgiji - na anaelewa ni kwanini mfumo wa nyota huyo wa Chelsea umevurugika kwa sasa. (Sun)

Chelsea imemfahamisha wakala wa Luke Shaw kuwa iko tayari kumsajili beki huyo wa Manchester United kama anataka kuondoka Old Trafford kwenye majira ya joto.

Tottenham inajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 40 kumnasa winga wa klabu ya Crystal Palace, Wilfried Zaha, lakini klabu hiyo ina amini kuwa thamani ya mchezaji wao ni kubwa zaidi ya hapo.

Mohamed Salah
Liverpool hawana nia ya kumuuza Mohamed Salah, hata kama Real Madrid itampa nyota huyo ofa ya mkataba wenye vigezo ambavyo hawana uwezo wa kuvimudu. (Daily Mail)

Manchester United wameulizia uwezekano wa kumsajili beki wa Arsenal, Hector Bellerin lakini Juventus inabaka kuwa klabu pekee inayopewa nafasi kubwa ya kumnasa raia huyo wa Uhispania.

Luke Shaw anahisi hajatendewa haki na Jose Mourinho na anafikiria kwenda moja kwa moja kulalamika mbele ya mkurugenzi mkuu klabu ya Manchester United, Ed Woodward.

Meneja wa Newcastle, Rafa Benitez amekataa kuanza mazungumzo juu ya kuongeza mkataba wake hadi atakapohakikishiwa kwamba atapewa pesa za kutosha kwa ajili ya usajili kwenye majira ya joto. (Mirror)

Steve McLaren amaeiambia Arsenal impe Eddie Howe kibarua cha kuinoa klabu yao achukue nafasi ya Arsene Wenger kwenye majira ya joto.

Jose Mourinho anafanya tathimini juu ya uhamisho wa kiungo wa klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey kwenye majira ya joto, ambaye bado hajafikia uamuzi wa kuongeza mkataba wake ambao unaisha mwaka 2019. (Star)

Toby Alderweireld
Paris Saint-Germain iko tayari kukabiliana na Manchester United pamoja na Barcelona kwenye mbio za kuwania saini ya beki wa klabu ya Tottenham, Toby Alderweireld baada ya Mbelgiji huyo kugoma kufanya mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake. (Telegraph)

Everton na Tottenham zinapewa nafasi kubwa ya kuweza kufanikisha uhamisho wa beki wa Manchester United, Luke Shaw kwenye majira ya joto. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 20 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 20 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/20/2018 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.