Zahera aeleza sababu ya kumtema Balinya
Balinya aliukosa mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1, bao la Yanga likifungwa na Patrick Sibomana katika dakika ya 25, huku bao la Zesco likifungwa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Thaban Kamusoko katika dakika ya 94'.
Akizungumzia suala hilo, Zahera amesema kuwa alimpumzisha mchezaji huyo ili apunguze uzito, ambapo hadi sasa amefanikiwa kupunguza takribani kilo nne.
“Nilimtaka apunguze kilo haraka, nimpongeze kwenye hilo na tatizo ndiyo sababu ya kwanza kumuweka benchi mchezo wetu na Zesco tuliocheza hapa nyumbani licha ya kuwa na mipango ya kutaka kumtumia kwenye mchezo wa marudiano,” amesema Zahera.
“Nataka wachezaji wawe na uzito sahihi ili watimize majukumu yao vyema wakiwa uwanjani, nilianza kwa Molinga (David). Baada ya hapo nilihamia kwa Balinya ambaye naye uzito uliongezeka kwa haraka mara baada ya ligi ya kwao kumalizika, nimefurahi kumuona akipunguza kilo nne kwa haraka", ameongeza.
Yanga inatarajia kusafiri Septemba 25 kuelekea nchini Zambia kucheza mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zesco.

Reviewed by Zero Degree
on
9/21/2019 07:50:00 AM
Rating: