Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 30 Julai, 2024


Arsenal wanavutiwa na mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen, klabu hiyo ya Italia huenda ikamuuza Osimhen kwa Chelsea kama sehemu ya mpango wa kubadilishana na Romelu Lukaku, na Everton wanakaribia kumsajili beki wa Lyon Jake O'Brien.

Arsenal bado wanamtaka mshambuliaji wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Nigeria Victor Osimhen, 25. (Corriere dello Sport)

Napoli pia wanavutiwa na mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 31, na huenda wakamjumuisha katika mkataba wa kubadilishana na Osimhen.

Mlinzi wa Jamhuri ya Ireland Jake O'Brien, 23, amewasili Merseyside kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya uhamisho wake wa pauni milioni 17 kutoka Lyon kwenda Everton. (Guardian)

Everton huenda wakawasilisha ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Strasbourg na Senegal Habib Diarra, 20. (L'Equipe)

Vilabu kadhaa kutoka Ligi ya Uingereza na nje ya nchi vinawania kumsajili winga wa klabu ya Luton Mholanzi Tahith Chong, mwenye umri wa miaka 24, kwa takriban £10m. (Sky Germany)

West Ham wanataka kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa na Monaco Youssouf Fofana, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anavutiwa na klabu ya AC Milan. (Givemesport)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 30 Julai, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 30 Julai, 2024 Reviewed by Zero Degree on 7/30/2024 08:11:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.