Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 7 Novemba, 2017

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho akiwa na golikipa wa timu hiyo, David de Gea
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho yuko tayari kumwachia David De Gea ajiunge na klabu ya Real Madrid endapo tu atapewa Raphael Varane kama sehemu ya ofa ya kumnasa golikipa huyo.

David Moyes ataanza kazi West Ham siku ya Jumanne kutuliza mioyo ya mashabiki wanaolalamikia uteuzi wake.

Anthony Martial amekiri kuumizwa na kitendo cha kupigwa benchi na kocha wa Manchester United. (Mirror)

Oguzhan Ozyakup
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anafanya mpango wa kutoa ofa ya paundi milioni 10 kumnasa nyota wa Besiktas na Uturuki, Oguzhan Ozyakup, ambaye alimuuza kwa paundi laki 4 mwaka 2012.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amewekwa katika orodha ya makocha wanaotarajiwa kuinoa Paris Saint-Germain.

Everton wanamtaka Sam Allardyce kama meneja wao mpya kwa kipindi kilichobaki hadi kumalizika kwa msimu huu.

Nyota anayewendwa na klabu ya Chelsea, Alex Sandro hataruhisiwa kuondoka mwezi Januari, hata kama vigogo hao watatoa ofa ya paundimilioni 53. (Sun)

David Moyes kutangazwa rasmi kama meneja mpya wa West Ham leo Jumanne kuzitikisa nguzo muhimu za klabu ambazo zilikuwa bado zina mapenzi na Slaven Bilic.

Tammy Abraham ameamua kusalia na na kikosi cha Uingereza licha ya kupewa nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria kinachotarajia kucheza kombe la dunia mwakani. (Daily Mail)

Danny Rose
Danny Rose atatetea nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoshiriki kombe la dunia licha ya kupoteza nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Tottenham Hotspur. (Telegraph)

Pep Guardiola (Manchester City) anamshangaa Arsene Wenger anavyodai Raheem Sterling ni mwongo.

Beki wa Leicester, Danny Simpson anasema kuwa meneja wao mpya, Claude Puel ameleta furaha katika kibarua chake. (Star)

David Moyes
David Moyes anatarajiwa kuwa na mwanzo mgumu kama meneja mpya wa West Ham, akifanya kazi na mwenyekiti msaidizi, Karren Brady ambaye hivi karibuni alimtuhumu kuwa ni mbaguzi wa jinsia.

Malky Mackay anaonekana kupoteza muda wake katika jitihada za kujaribu kumtengeza winga Matt Phillips kuwa msahmbuliaji wa Scotland. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 7 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 7 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/07/2017 10:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.