Loading...

Rais Samia amemteua Magambo kuwa Mkurugenzi Mkuu PSSSF


Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Fortunatus Magambo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi za Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Fortunatus Magambo

Kabla ya uteuzi huu, ambao umetangazwa Alhamisi, Desemba 11, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu, Bakari Machumu, Magambo alikuwa Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi ndani ya mfuko huo.

Wakati huo huo, Rais Samia pia amemteua Plasduce Mbossa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Plasduce Mbossa

Mbossa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), anachukua nafasi ya Dk Rhimo Nyansaho, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu



Rais Samia amemteua Magambo kuwa Mkurugenzi Mkuu PSSSF Rais Samia amemteua Magambo kuwa Mkurugenzi Mkuu PSSSF Reviewed by Zero Degree on 12/11/2025 04:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.