Loading...

Freeman Mbowe aachiwa huru baada ya kuhojiwa

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameachiwa saa saba na robo usiku wa kuamkia leo baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi.

Mbowe alikamatwa jana Jumatatu jioni wakati akienda kujisalimisha polisi na kupekuliwa nyumbani kwake kabla ya kuhojiwa hadi alipoachiwa usiku.

Ofisa habari wa chama hicho, Tumaini Makene ameithibitishia Mwananchi Digital taarifa za kuachiwa mwanasiasa huyo kuwa ni za kweli.

Hata hivyo, taarifa iliyosambazwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu kupitia mitandao ya kijamii imesema kuwa chama hicho kitatoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo leo.

“Tunawashukuru wote kwa sala, maombi na subira na hivyo kuhitimisha salama saa kumi za mwenyekiti wetu kuwa chini ya Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam,” Mwalimu amesema.
Freeman Mbowe aachiwa huru baada ya kuhojiwa Freeman Mbowe aachiwa huru baada ya kuhojiwa Reviewed by Zero Degree on 2/21/2017 01:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.