Loading...

Mpizani wa Rais Paul Kagame nchini Rwanda atangaza serikali mbadala

Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, ametangaza kuunda serikali sambamba na utawala uliopo Rwanda, lakini itakayokuwa ikifanya kazi nje ya nchi.

Thomas Nahimana ambaye ni kasisi wa zamani anayeishi nchini Ufaransa ametangaza kuunda serikali hiyo itakayofanyia kazi uhamishoni.

Katika mazungumzo na BBC, mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza wananchi.

Thomas Nahimana, amekatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Baraza lake la mawaziri

Ametangaza tayari baraza lake la mawaziri.

Baadhi ya aliowataja katika baraza lake la mawaziri ni wafungwa wanaotumukia vifungo vya jela nchini Rwanda kwa makosa kama vile kukanusha kuwa mauwaji ya kimbari hayakufanyika nchini Rwanda mwaka 1994.

Nahimana (kushoto) akiwa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mwaka jana ambapo alizuiwa kwenda Rwanda
Nahimana, ambaye ni mhutu, amelaumiwa kwa kuandika taarifa kadhaa za kikabila na kumkosoa rais Paul Kagame.

Chama chake cha Ishema, bado hakijaandikishwa nchini Rwanda.
Mpizani wa Rais Paul Kagame nchini Rwanda atangaza serikali mbadala Mpizani wa Rais Paul Kagame nchini Rwanda atangaza serikali mbadala Reviewed by Zero Degree on 2/21/2017 10:02:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.