Fumanizi la Mapenzi: Hii ni Riwaya ya kusisimua itakayokupa maana halisi ya Mapenzi na athari zake
MTUNZI: MC Short Charles Gwimo
Utangulizi:
Tafsiri sahihi ya neno mapenzi imejikita katika hali ya kuingiwa moyoni na kuthamini mtu au kitu zaidi ya mwingine au kitu kingine. Kwa upande mwingine mapenzi yametafsiriwa kama nyovida, Mahaba n.k. Fumanizi la Mapenzi ni moja ya Riwaya pendwa inayoibua maana halisi ya Mapenzi na athari zake endapo yatatumika kinyume na utaratibu halali. Mapenzi ni zawadi maalum toka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake. Zawadi hii ya Mapenzi, hakuwa na malengo kwamba yatumike Sekemnege bali yafuate utaratibu maalumu. Na kwa hilo hakuwa mfichi wa namna ya matumizi ya mapenzi kwani katika vitabu vyake vitakatifu na vile vitukufu anawaasa waja wake. Wasiikaribie zinaa bali waikimbie na kuwa mbali nayo.

*******
Fumanizi la Mapenzi inamwibua kijana David Sikitiko aliyefumwa na Mapenzi na kujikuta akisahau majukumu yake katika familia na kuwa limbukeni asiyejua zuri wala baya katika kuyawakilisha mawazo na hisia ya mapenzi. Wajihi na Ukwasi wa kijana David ni moja ya mambo ambayo yalimfanya apapatikiwe na watoto wa kike na hasa wale waliojikita kwenye kundi la mapenzi pesa kuolewa ni ushamba. Ukwasi na mwonekano wa kijana David, unamfanya ashindwe kuwa na chaguo sahihi la kudumu na mwenzi wa maisha yake lakini anajikuta anakuwa mmahiri katika tasnia ya mapenzi bila kupitia shule au chuo chochote cha mapenzi.
Kutokana na hilo la kuwa mmahiri, amejikuta akikabidhiwa majina pasi na ubatizo maalumu kama vile Kijogoo, Kijeba na hata wengine kumuita Mkaguzi jina ambalo limemkaa sawa sawia kutokana na vitendo vyake vya kutokukaa na mtoto wa kike zaidi ya siku moja. Kama ni njia alizijua sawa sawa kama mkaguzi kwani alizijua zenye tope, bomba mvua, mnato, mbano, na mdomo wa bata. Aliwajua wenye bambataa za kichina na zile za asili, wenye maumbo ya namba zero, moja na ile namba maarufu ipendwayo na wengi yaani umbo namba nane. Alifanikiwa kuwarubuni watoto chini ya umri yaani wanafunzi, alivunja ndoa za watu lakini hata yeye hakufanikiwa kuujenga mji wake zaidi ya kutapanya watoto kila kona ambao hakuwajua kwa hali hata kwa mali kwa uzima hata maradhi.

Huyu ndiye kijana David Sikitiko asiyejua thamani ya mapenzi na athari zake zaidi ya kuyachukulia mapenzi kama tendo la kumburudisha mwenye kiu ya mapenzi. Mapenzi ni kitu gani? Kwa wengine Raha na wengine Karaha. Ungana na mtunzi wako MC Short Charles Gwimo ili upate uhondo wa simulizi ya Fumanizi la Mapenzi mwanzo hadi mwisho.
Usikubali kupitwa na Sehemu yoyote kuanzia ya kwanza hadi ya mwisho, kwani ni Simulizi yenye radha mpya na imeandikwa na mtunzi aliyebobea katika tasnia hii. Sehemu ya kwanza ya Simulizi ya FUMANIZI LA MAPENZI itakujia siku ya Ijumaa Tarehe 2 juni, 2017. Hutajutia kuifuatilia simulizi hii kwani niya kusisimua pia iliyojaa mafundisho na itakuwa ndio mara yako ya kwanza kuiona Simulizi hii na ni hapa Zero Degree pekee.
Fumanizi la Mapenzi: Hii ni Riwaya ya kusisimua itakayokupa maana halisi ya Mapenzi na athari zake
Reviewed by Zero Degree
on
5/31/2017 09:28:00 AM
Rating: