Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 6 Novemba, 2017
Conte na David Luiz wakiwa mazoezini |
Antonio Conte alimuacha David Luiz nje ya kikosi kilichoibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Manchester United Jumapili na kuonya kwamba, jambo kama hilo linaweza kumkumba mchezaji yeyeto wa Chelsea.
David Moyes atapewa nafasi ya kurejea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza wiki hii katika klabu ya West Ham baada ya kukubali mkataba wa kukinoa kikosi hicho hadi mwisho wa msimu huu.
Riyad Mahrez |
Roma wamethibisha kwamba Barcelona walikuwa wapinzani wao wakubwa waliokwamisha mpango wao wa kumsajili nyota wa Leicester, Riyad Mahrez katika kipindi cha majira ya joto.
Sadio Mane anaamini kwa kushirikiana na Mo Salah wanaweza kuibeba klabu ya Liverpool kwa sababu wamefanya hivyo pia kwa timu zao za taifa.
Golikipa wa ziada wa klabu ya Watford, Costel Pantilimon amepewa ruhusa ya kuondoka mwezi Januari.
Klabu za Watford na Brighton zote zinatarajiwa kujaribu kunsajirli beki wa klabu ya Portsmouth, Matt Clarke. (Mirror)
Rais wa Bayern Munich, Karl-Heinz |
Bayern Munich wameamua kumpotezea Alexis Sanchez kufuatia Rais wa klabu hiyo, Karl-Heinz Rummenigge kudai kwamba mshambuliaji huyo wa Arsena, tayari ameshachagua klabu anayoitaka.
Marouane Fellaini ameifungulia mashtaka kampuni ya New Balance akidai kulipwa fidia ya zaidi ya paundi milioni 2 kwa kutuhumu viatu vya kampuni hiyo, ambapo amedai kwamba viatu vyao vimemsababishia madhara makubwa kwenye miguu. (Daily Mail)
Thomas Meunier amesema aliipotezea ofa ya kujiunga na Chelsea licha ya kupoteza nafasi yake PSG kwa Dani Alves.
Rangers wanatazamia kufanya mazungumzo na aliyekuwa meneja wa zamani wa Uingeleza, Steve McClaren juu ya kibaru cha kuinoa klabu hiyo. (Sun)
Mauricio Pochettino amekubaliana na meneja wa Uingereza, Gareth Southgate kutomtumikisha sana mshambuliaji wake, Harry Kane.
Liverpool wana mpango wa kufanya usajili wa kushitukiza wa winga wa klabu ya Manchester City, David Silva, ambaye bado hajakubali kusaini mkataba mpya na ikiwa mkataba wake wa sasa unaisha mwisho wa msimu huu.
Demarai Gray anavizia kupewa nafasi kwenye kikosi cha Timu ya taifa ya Uingereza baada ya kufanikiwa kuwa tegemezi katika kikosi cha Claude Puel, Leicester City. (Telegraph)
Mauricio Pochettino amekubaliana na meneja wa Uingereza, Gareth Southgate kutomtumikisha sana mshambuliaji wake, Harry Kane.
Tony Pulis anaamini kwamba bodi ya West Brom bado ina imani naye licha ya kuchapwa goli 1-0 na Huddersfield wikendi iliyopita.
Sam Vokes ana shauku ya kuona meneja wa klabu ya Burnley, Sean Dyche anasalia na kikosi hicho.
Meneja wa Stoke City, Mark Hughes amemwambia Peter Crouch kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumuuza kwa dau lolote lile. (Star)
Winga wa Manchester City, David Silva |
Andy Carroll amewanyoshea kidole mashabiki kufuatia kuboronga kwa klabu yao na kusistiza kwamba jambo hilo litaikwamisha West Ham. (Express)
Demarai Gray anavizia kupewa nafasi kwenye kikosi cha Timu ya taifa ya Uingereza baada ya kufanikiwa kuwa tegemezi katika kikosi cha Claude Puel, Leicester City. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 6 Novemba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
11/06/2017 02:23:00 PM
Rating: