Loading...

Watuhumiwa 16 wa madawa ya kulevya wakamatwa mkoani Kagera.

Picha ya Mtandao: Moja ya shamba la bangi likiteketezwa kwa moto
Jeshi la polisi kwa kushirikiana na jeshi la wananchi Tanzania,Magereza na uhamiaji wilaya ya Karagwe mkoani Kagera linawashikilia watuhumiwa wa madawa ya kulevya 16 wakiwemo watendaji wa serikali za vijiji wanaojihusisha na biashara haramu katika mpaka wa Tanzania na nchi ya Rwanda kinyume cha sheria za nchi.

Kundi hilo la wananchi wa kijiji cha Muguruka kata ya Bweranyange wilaya ya Karagwe wakiapa kutoendelea na biashara haramu ya usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya ndani na nje ya nchi baada ya kukamatwa na kuhojiwa mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Karagwe ambapo wengi wao wamekili kutoendelea na biashara hiyo huku mmoja wa wakulima wa dawa za kulivya aina ya bangi akiwashangaza watu kwa kusema kwamba anapotumia dawa za kulevya hupata nguvu nyingi za kulima shamba.

Akizungunza baada ya kuteketeza kwa moto shamba la dawa za kulevya aina ya bangi zaidi ya hekari 40 mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Karagwe Bw.Godfrey Mheluka ameiomba serikali kupitia jeshi la polisi kuwaazimisha ndege ndogo aina ya chopa kwa lengo la kuwezesha kuvifikia visiwa vinne vinavyozungukwa na mto Kagera ambavyo havifikiki zaidi ya ndege ambapo inasadikiwa kuwa visiwa hivyo vimesheheni mashamba makubwa ya bangi zinazouzwa ndani na nje ya nchi.

Source: ITV
Watuhumiwa 16 wa madawa ya kulevya wakamatwa mkoani Kagera. Watuhumiwa 16 wa madawa ya kulevya wakamatwa mkoani Kagera. Reviewed by Zero Degree on 2/12/2017 05:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.