Loading...

Alichojibu Mrisho Ngassa baada ya kuulizwa nani atakayebeba Ubingwa wa VPL msimu huu wa 2016/17

MSHAMBULIAJI wa Mbeya City Mrisho Ngasa amesema hivi sasa huwezi kutabiri nani bingwa kutokana na timu zote (Simba na Yanga) kuwa katika nafasi nzuri za kugombani nafasi hiyo.

Ngasa alicheza Yanga kwa mafanikio makubwa kabla ya kusajiliwa na Free State ya Afrika kusini na baadae kuibukia katika klabu ya Fanja ya Oman kabla ya kurudi bongo na kujiunga na Mbeya City.

Mrisho Ngasa, aambaye alisema ligi ya msimu huu huwezi kujua nani anachukua kombe kama tulivyokuwa tumezoea zamani kuwa timu inatangaza ubingwa ikiwa ina mechi kadhaa mkononi.

“Siyo Yanga wala Simba yoyote atakaecheza vizuri na kupata matokeo ndani ya uwanja ndiyo atafanikiwa kuwa bingwa msimu huu,” alisema Ngasa.

Ngasa ambae ameshacheza kwenye vilabu vitano tofauti vya ligi kuu Tanzania bara ambavyo ni Kagera Sugar, Yanga, Azam, Simba na sasa Mbeya City. Lakini alipata mafanikio ya juu wakati akiwa Yanga SC.

Source: ShaffihDauda
Alichojibu Mrisho Ngassa baada ya kuulizwa nani atakayebeba Ubingwa wa VPL msimu huu wa 2016/17 Alichojibu Mrisho Ngassa baada ya kuulizwa nani atakayebeba Ubingwa wa VPL msimu huu wa 2016/17 Reviewed by Zero Degree on 3/05/2017 08:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.