Loading...

Yanga nayo yashindwa kufurukuta kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro

 Yanga imeshindwa kufika kileleni baada ya sare ya bila kufungana dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, leo.

Ilikuwa mechi yenye mvuto na Yanga watajilaumu baada ya kupata penalti dakika ya 33, lakini Simon Msuva akapiga shuti kuubwa juu ya lango la Mtibwa Sugar.

Msuva akijishika kichwa baada ya kukosa penati
Sare hiyo, inaifanya Yanga kufikisha pointi 53 hivyo kuiacha Simba ikiendelea kutamba kileleni na pointi zake 55 baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Mbeya City, jana.
Yanga nayo yashindwa kufurukuta kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro Yanga nayo yashindwa kufurukuta kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro Reviewed by Zero Degree on 3/05/2017 08:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.