Loading...

Mwanaharakati aliyefungwa jela pamoja na Mandela, Ahmed Kathrada afariki dunia

Nelson Mandela akiwa na Ahmed Kathrada mwaka 1990, muda mfupi baada ya kutoka gerezani [Picha ya mtandao]
Kiongozi mwanaharakati aliyeshiriki sana kupigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Ahmed Kathrada amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87, wakfu wake umetangaza.

Bw Kathrada alifariki dunia akiwa katika hospitali moja mjini Johannesburg "baada ya kuugua kwa muda mfupi, kufuatia upasuaji aliofanyiwa kwenye ubongo wake".

Ahmed Kathrada enzi za uhai wake
Pamoja na Nelson Mandela, Bw Kathrada alikuwa miongoni mwa wanaharakati wanane wa African National Congress waliohukumiwa kufungwa jela maisha mwaka 1964.

Walipatikana na hatia ya kujaribu kupindua serikali ya ubaguzi wa rangi.

Bw Kathrada alikaa jela miaka 26, 18 kati ya miaka hiyo akiwa katika gereza hatari la Robben Island.

Aliachiliwa huru mwaka 1989.

Rais Mandela baadaye alimshawishi kujiunga na serikali.

Ahmed Kathrada aliondoka bungeni 1999, lakini aliendelea kushiriki katika siasa nchini humo.

Alikosoa mwelekeo wa chama cha ANC hivi majuzi na kumtaka Rais Jacob Zuma kujiuzulu.
Mwanaharakati aliyefungwa jela pamoja na Mandela, Ahmed Kathrada afariki dunia Mwanaharakati aliyefungwa jela pamoja na Mandela, Ahmed Kathrada afariki dunia Reviewed by Zero Degree on 3/28/2017 10:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.