Loading...

Wenger maji yamfika shingoni

Arsene Wenger atatangaza 'muda si mrefu' kama atabaki kuwa kocha wa Arsenal au ataondoka baada ya kufikia uamuzi.

Kocha huyo wa Gunners alizungumza hivyo baada ya mchezo wa kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya West Brom, kikiwa ni kichapo cha nne katika mechi tano za Ligi Kuu England.

Kipigo hicho kiliongeza presha kwa kocha huyo wa Ufaransa na kuiacha Arsenal ikiwa katika hatihati ya kupoteza nafasi nne za juu kwa mara ya kwanza tangu alipoichukua timu hiyo 1996. "Ninajua kitu gani nitafanya," amesema Wenger. "Muda si mrefu hili litakuwa wazi na mtalifahamu, subirini."
Wenger maji yamfika shingoni Wenger maji yamfika shingoni Reviewed by Zero Degree on 3/20/2017 11:09:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.