Askari bandia atiwa mbaroni na Jeshi la Polisi jijini Dar
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar as Salaam linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Paulo Baruti kwa kosa la kuvaa sare za Jeshi la Polisi na kuwalazimisha wananchi kumnunulia pombe na kuwatishia kuwafikisha kituo cha polisi kama wangekataa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 12,2017, Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro amesema katika mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kutumia sare hizo za polisi kimakosa ambazo ni za kaka yake aitwaye Lyanga Baruti ambaye ni askari polisi.
“Mtuhumiwa alikamatwa Aprili 8,2017 maeneo ya Tandale uwanja wa fisi, katika mahojiano alikiri kutumia sare hizo ambazo ni za kaka yake ambaye ni askari polisi na kwa sasa yuko likizo kwao Mpanda mkoani Katavi,” amesema.
Kamanda Sirro amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini kama mtuhumiwa ni mara yake ya kwanza kufanya tukio hilo na kama hajawahi kushiriki katika matukio ya ujambazi kwa kutumia sare hizo.
Aidha, mtuhumiwa huyo alieleza mbele ya waandishi wa habari jinsi alivyopata sare hizo na kusema kuwa alizichukua kutoka katika chumba cha kaka yake.
“Hizi nguo ni za kaka yangu yuko hapa Kanda Maalumu, nilizichukua jumamosi saa tatu usiku,” amesema.

Reviewed by Zero Degree
on
4/12/2017 11:50:00 PM
Rating: