Loading...

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi [Tucta] kuipeleka serikali mahakamani

Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya
Tucta imeitaka serikali kusitisha makato ya asilimia 15 kama malipo ya mkopo wa elimu ya juu na kurudi kiwango cha awali cha asilimia nane kinyume na hapo wataipeleka mahakamani.

Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya alisema Baraza kuu la shirikisho hilo limesharidhia uamuzi huo na tayari lipo kwa wanasheria.

"Wanasheria wetu wanalifanyia kazi na kuendelea kukusanya nyaraka zitakazotusaidia,muda wowote kuanzia wiki Idaho tutalifikisha suala hili mahakamani," alisema

Alisema ameendelea kupata malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi kutokana na makato hayo ikilinganishwa na hali ngumu ya maisha ilivyo sasa.

Source: Mwananchi
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi [Tucta] kuipeleka serikali mahakamani Shirikisho la vyama vya wafanyakazi [Tucta] kuipeleka serikali mahakamani Reviewed by Zero Degree on 4/12/2017 11:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.