Loading...

Dola 120 milioni zaidhinishwa kutumika kwenye uchaguzi mpya Kenya


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameidhinisha mswada wa bajeti ndogo ambao umetenga Kshs 12 bilioni (Dola 120 milioni) za kutumiwa na Tume ya Uchagizi katika uchaguzi mkuu mpya tarehe 26 Oktoba.

Kadhalika, kutengwa kwa Kshs 25 bilioni za kutumiwa kufadhili mpango wa elimu ya sekondari bila malipo ambao Rais Kenyatta alikuwa ameahidi kwenye kampeni kwamba utaanza kutekelezwa Januari mwaka ujao.

Aidha, kuna Kshs 6.7 bilioni za kufadhili ununuzi wa mahindi kuhakikisha kuuzwa kwa unga wa bei nafuu.

Wazee wa miaka 70 na zaidi wametengewa Kshs 6.7 bilioni chini ya mpango wa Inua Jamii ambao hutoa malipo kila mwezi kuwasaidia kujikimu kimaisha.

Idara za usalama zimetengewa Kshs 4 bilioni kwenye bajeti hiyo ndogo iliyoidhinishwa.

Serikali pia imetenga Kshs 3.9 bilioni za kukabiliana na athari za ukame.
Dola 120 milioni zaidhinishwa kutumika kwenye uchaguzi mpya Kenya Dola 120 milioni zaidhinishwa kutumika kwenye uchaguzi mpya Kenya Reviewed by Zero Degree on 10/13/2017 02:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.