Loading...

Sababu ya Conte kutaka kuondoka Chelsea yabainika


Conte amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Chelsea miezi kadhaa iliyopita.

Katika msimu wa 2016/17, mambo yalikua mazuri kwa Chelsea kwa kufanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu chini ya uongozi wa meneja mpya Antoni Conte, lakini mambo hayajawa vizuri ndani ya klabu ya Chelsea tangu watwae taji hilo.

Kwa kushindwa kupata matokeo mazuri kwenye fainali ya FA Cup dhidi ya Arsenal, Conte alikuwa na mpango wa kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi chake cha kwanza na alitarajia kuingiza nguvu mpya ya kutosha kikosini.

Conte alitazamia kusajili wachezaji wazuri kutoa barani Ulaya kuisaidia Chelsea kwenye michuano ya Klabu Bingwa msimu huu lakini taarifa zinadai kwamba meneja huyo hakubaliani ni Bodi ya klabu juu ya taratibu za uhamisho zilizotumika katika majira ya joto.

Kwa mujibu wa taarifa mbali mbali, meneja huyo wa Chelsea yuko kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu na anakaribia kuondoka Stamford Bridge.

Mtandao wa 'As.com' umethibitisha kwamba, Fernando Llorente ndiye aliyekuwa chaguo la kwanza la muitaliano huyo ambaye alikuwa ameuomba uongozi wa Klabu ya Chelsea umsajili mshambuliaji huyo, lakini ombi lake halikutimizwa.

Chelsea walitoa ofa ya paundi milioni 5.5 kumnasa nyota huyo wa zamani wa Klabu ya Juventus aliyefunga magoli 16 kwenye Serie A chini ya uongozi wa Conte.

Hatimaye Llorente akawa amejiunga na Tottenham kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 10.
Sababu ya Conte kutaka kuondoka Chelsea yabainika Sababu ya Conte kutaka kuondoka Chelsea yabainika Reviewed by Zero Degree on 10/13/2017 02:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.