Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 7 Januari, 2018

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Wales na Real Madrid, Gareth Bale
Manchester United watakumbana na ushindani kutoka klabu ya ligi kuu ya China kama Real Madrid watamuuza Gareth Bale.

Real Madrid wamembiwa kwamba watalazimika kulipa kiasi cha pauni milioni 300 ili kumpata Harry Kane kutoka Tottenham.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anaweza kukatisha mkataba wake wa sasa na kuingia kwenye bodi ya klabu kwenye majira ya joto na angependelea nafasi yake ichukuliwe na Mikel Arteta.

Arsene Wenger atamwacha Alexis Sanchez ajiunge na Manchester City kwa pauni milioni 35 mwezi huu - ikiwa ataweza kusajili Riyad Mahrez achukuwe nafasi yake.

Jose Mourinho ataushangaza ulimwengu kwa kumsajili Mesut Ozil kutoka Arsenal mwezi huu.

Sam Allardyce anategemea kutumia pauni milioni 50 kunasa wachezaji wawili mwezi huu - huku beki wa klabu ya Swansea, Alfie Mawson na kiungo wa klabu ya Watford, Abdoulaye Doucoure wakiwa kwenye mipango yake.

Danny Ings
Meneja wa Newcastle, Rafa Benitez anasubiria mipango ya bajeti yake ya usajili katika msimu huu wa baridi, akiwania saini mshambuliaji wa Liverpool, Danny Ings. (Mirror)

Liverpool kurejesha fedha kwa mashabiki walionunua jezi za Phillipe Coutinho kwa msimu huu wa 2017/18

Mirallas amekubali kurejea katika klabu ya Olympiakos kwa mkopo, ambako aliicheza kwa muda wa miezi 15 kabla ya kusaini Everton.

Klabu ya Liverpool haina nia ya kumsajili nyota wa Leicester City, Ryad Mahrez mwezi huu. (Sky Sports)

Stoke City wamfukuza kocha wao Mark Hughes baada ya kupoteza mechi kwenye michuano ya FA.

Liverpool wamebaki njia panda baada ya kummuza nyota wao Phillipe Coutinho kwenda Barcelona.

Southampot wanamtaka nyota wa klabu ya Arsenal, Theo Walcot. (ESPN)

Eden Hazard anatarajiwa kukataa ofa ya Real Madrid na kusaini mkataba mpya utakaomfanya awe mchezaji wa EPL anayelipwa fedha nyingi zaidi.

Inter Milan wamepata Bonasi nzuri ya Chistmas kufuatia uhamisho mkubwa wa Philippe Coutinho kutoka Liverpool kwenda Barcelona. (Express)

West Ham wako tayari kutoa ofa ya pauni milioni 25 kwa ajili ya uhamisho wa beki wa Swansea, Alfie Mawson.

Sam Allardyce anahitaji straika mpya - na kwenye orodha yake, Diafra Sakho na Moussa Dembele ndio wako mstari wa mbele.

Harry Maguire
Manchester City wanamtaka Harry Maguire kutoka Leicester na wako tayari kutoa ofa ya pauni milioni 50.


Crystal Palace wanafanya mpango wa kushitukiza usajili wa mshambuliaji wa  Watford, Stefano Okaka.

Rangers wana matumaini ya kufanikiwa kushinda kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya mshambuliaji wa Fleetwood, Devante Cole.

Nyota anayewindwa na klabu ya Aston Villa, Nick Powell atasaini mkataba mpya Wigan na kubakia katika klabu yake - endapo mabadiliko ya kudumu kwenye umiliki wa klabu hiyo yatafanikiwa. (Sun)

Sheffield United wanakaribi kukamilisha taratibu za uhamisho wa kiungo wa klabu ya Wolves na raia wa Wales, Lee Evans.

Newcastle wanafanya mpango wa kumsajili golikipa kutoka PSG, Kevin Trapp kwa mkopo. (Daily Mail)

Fred
Manchester United na Arsenal zimeingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya Mbrazil, 
Fred anayekipiga katika klabu ya Shakhtar Donetsk. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 7 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 7 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/07/2018 10:41:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.