Loading...

66 wafariki kwenye ajali ya ndege Iran


Watu 66 wamefariki papo hapo kwenye ajali mbaya ya Ndege iliyotokea leo asubuhi huko nchini Iran baada ya kuanguka mlimani.

Ndege hiyo yenye namba ATR-72 iliyokuwa ikisafiri kutoka Tehran kwenda jijini Yasuj imedondoka katika milima ya Semirom iliyopo kusini mwa Iran.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari la AP, Watu wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamefariki huku chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.
66 wafariki kwenye ajali ya ndege Iran 66 wafariki kwenye ajali ya ndege Iran Reviewed by Zero Degree on 2/18/2018 04:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.