Loading...

Conte: Huu ndio udhaifu mkubwa wa Barcelona

Antonio Conte
Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte anahisi kuwa klabu yake itaifunga Barcelona siku ya Jumanne.

'The Blues' itawakaribisha vigogo hao wa La Liga kwenye dimba la Stamford Bridge siku ya Jumanne kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora.

Antonio Conte ansema kuwa ametumia mwezi mmoja uliopita kuchunguza mapungufu anayoweza kuyatumia kukabiliana na klabu ya Barcelona. 

Meneja huyo anasema Chelsea itatakiwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu sana ili kusonga mbele zaidi na ana amini kuwa vijana wake watakuwa na madhara makubwa pale watakapokuwa na mpira.

Conte alisema: “Tumekuwa tukiifanyia timu hii uchunguzi kwa muda mrefu. Tulianza uchunguzi huo mwezi mmoja uliopita.

“Tunazungumzia moja kati ya timu bora zaidi duniani. Lazima tujaribu kucheza mchezo wa hali ya juu na kujaribu kuwa na maamuzi bora zaidi kwa timu kama hii.

“Hawa ni wapinzani tofauti kabisa. Wana sifa ya ajabu pale wanapomiliki mpira, lakini wana weza kuwa na mapungufu pale wanapokuwa bila mpira na lazima tujaribu kuitumia nafasi hii.”

Lionel Messi ameshindwa kufunga goli katika mechi nane alizocheza dhidi ya Chelsea – rekodi yake mbaya zaidi dhidi ya timu moja katika soka.

“Natumaini kuwa tutaitunza tamaduni hii, lakini hapa tunamzungumzia mchezaji mwenye uwezo wa hali ya juu,” alisema Conte

“Lazima tuwe na heshima kubwa na wakati huo huo lazima tuwe makini katika kukabiliana na mpinzani kama huyu.

“Haitakuwa rahisi kwa sababu tunatambua vizuri uwezo wa mchezaji huyu, hapa tunamzungumzia mmoja kati ya wachezaji bora zaidi duniani.

“Lakini nina uhakika kwamba tutacheza kwa umoja, tutafanya kazi na timu nzima, lakini si tu kwa kumdhibiti yeye peke yake.

“Kama tutacheza kwa kumtazama Messi peke yake, tunaweza kujiweka katika hatari kubwa.”
Conte: Huu ndio udhaifu mkubwa wa Barcelona Conte: Huu ndio udhaifu mkubwa wa Barcelona Reviewed by Zero Degree on 2/18/2018 06:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.