Loading...

Rais Magufuli aagiza waliosababisha kifo cha mwanafunzi wa NIT wachukuliwe hatua


Rais wa Tanzania John Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuchunguza na kuwachukulia hatua waliosababisha kifo cha mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji Tanzania, NIT, Akwilina Akwiline.

"Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT). Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu. Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili," Rais Magufuli aliandika kwenye mtandao wa Twitter.

Mwanafunzi huyo ambaye jina lake na picha vilisambazwa katika mitando ya kijamii alipigwa risasi akiwa ndani ya basi dogo maarufu kama daladala jijini Dar es salaam, siku ya Ijumaa majira ya jioni, ikiwa siku moja kabla ya uchaguzi mdogo wa eneo bunge la kinondoni kufanyika.

Soma zaidi: 
Walioshuhudia wanasema kuwa maafisa wa polisi walitumia vitoa machozi na risasi katika harakati za kuwatawanya mamia ya wafuasi wa chama cha Chadema waliokuwa wakiandamana hadi afisi za tume ya uchaguzi.

Wakati huo huo mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP), wamemtaka waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba kujiuzulu kutokana na tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Akwilina Akwilini.

Taaria zaidi pia zinasema kuwa polisi 6 wamekamatwa kwa tuhuma za kutumia risasi za moto wakati wa uchaguzi mdogo mjini Dar es Salaam.
Rais Magufuli aagiza waliosababisha kifo cha mwanafunzi wa NIT wachukuliwe hatua Rais Magufuli aagiza waliosababisha kifo cha mwanafunzi wa NIT wachukuliwe hatua Reviewed by Zero Degree on 2/18/2018 06:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.