Loading...

Mwanafunzi afariki dunia baada ya kupigwa risasi

Akwilina Akwilini
Makabiliano kati ya jeshi la polisi na wafuasi wa chama cha Chadema nchini Tanzania yalisababisha kifo cha mwanafunzi mmoja wa shule.

Mwanafunzi huyo wa chuo cha usafirishaji Tanzania NIT ambaye jina lake na picha vilisambazwa katika mitando ya kijamii alipigwa risasi akiwa ndani ya basi dogo maarufu kama daladala jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa majira ya jioni, ikiwa siku moja kabla ya uchaguzi mdogo wa eneo bunge la kinondoni kufanyika.

Walioshuhudia wanasema kuwa maafisa wa polisi walitumia vitoa machozi na risasi katika harakati za kuwatawanya mamia ya wafuasi wa chama cha Chadema waliokuwa wakiandamana hadi afisi za tume ya uchaguzi.

Baadhi ya wanachama wa chama hicho walikamatwa.

Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Zacharia Mganilwa alithibitisha kuwa mwanafunzi wao wa shahada ya Manunuzi na Ugavi, Akwilina Akwilini alifariki dunia siku ya Ijumaa.

Amesema kuwa mwili wa msichana huyo ulikuwa na jeraha la risasi kichwani.

Kwa mujibu wa uongozi wa chuo hicho, mwanafunzi huyo alikuwa safarini kulekea Bagamoyo kupeleka fomu za kuomba nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo mjini Bagamoyo.


Kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa
Jeshi la Polisi limehusishwa na kifo hicho na tayari kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na Polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao anasema walizua fujo na kufunga barabara za mabasi ya mwedo kasi.

Polisi walitumia vitoa machozi na risasi kuwatawanya na moja kati ya risasi zilizopigwa hewani ilimpata mtu.

Kamanda Mambosasa licha ya kutoa uthibitisho huo hajaweka wazi iwapo mtu huyo ndiye mwanafunzi huyo wa chuo Chuo cha usafirishaji Tanzania NIT

Tanzani hii leo inafanya uchaguzi mdogo katika maeneo bunge mawili baada ya wabunge wa maeneo hayo ambayo yalikuwa yakishikiliwa na wabunge wa CUF na CHADEMA kujiuzulu kwa kile walichokiita kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano kuiletea Tanzania maendeleo.
Mwanafunzi afariki dunia baada ya kupigwa risasi Mwanafunzi afariki dunia baada ya kupigwa risasi Reviewed by Zero Degree on 2/17/2018 08:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.