Loading...

Mjerumani anayeinyima Arsenal usingizi huyu hapa

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger
Arsenal imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig na Timu ya Taifa ya Ujeruman, Timo Werner.

Mshambuliaji huyo ambaye tayari anawaniwa na Chelsea, Manchester United na Liverpool, amekataa kusaini mkataba mpya na klabu yake ya sasa.

Wenger alifikia hatua ya kutuma mtu akamfuatilie raia huyo wa Ujerumani kwenye mechi ya Ligi ya Europa dhidi ya Napoli.

Timo Werner, 21
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kuja kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu Ujerumani. Ameshafunga magoli 15 katika mechi 24 za michuano yote msimu huu, ikiwa ni pamoja na magoli matatu ya Ligi ya Mabingwa.


Ameshaichezea Timu ya Taifa ya Ujerumani mechi 10, na kufunga magoli saba.

Ukiachana na ushindani kutoka kwa wapinzani wa Ligi Kuu ya Uingereza, washika bunduki pia watalazimika kushindana na Real Madrid pamoja na Atletico Madrid kuwania ya saini mshambuliaji huyo.
Mjerumani anayeinyima Arsenal usingizi huyu hapa Mjerumani anayeinyima Arsenal usingizi huyu hapa Reviewed by Zero Degree on 2/17/2018 10:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.