Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 17 Februari, 2018

Victor Wanyama akishangilia goli pamoja na Harry Kane
Liverpool inamfuatilia kiungo wa klabu ya Tottenham, Victor Wanyama, huku sakata la mkataba mpya wa Emre Can likiendelea kuwa gumu Anfield.

Ousmane Dembele anaweza kuondoka katika klabu ya Barcelona mwishoni mwa msimu huu na Arsenal ikiwa ndio klabu pekee inayopewa nafasi kubwa kumnasa kiungo huyo. (Star)

Meneja wa klabu ya Tottenham, Murcio Pochettino amekataa kuzungumzia juu ya tetesi za uhamisho wa beki wa klabu hiyo, Toby Alderwiereld.

Michy Batshuayi amesema kuwa anahisi kuaminiwa katika klabu ya Borussia Dortmund kuliko ilivyokuwa kwa Chelsea. (talkSport)

Meneja wa klabu ya West Brom, Alan Pardew anakiri kuwa hana uhakika wa kuendelea na kibarua cha kuinoa klabu hiyo.

Beki mkongwe wa klabu ya Birmingham, Paul Robinson atatundika daruga mwisho wa msimu huu.

Klabu ya Real Madrid haina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa, Paul Pogba.

Jose Mourinho anasema kuwa klabu ya Manchester United inahitaji kiungo mwingine atakayechukuwa nafasi ya Michaek Carrick, ambaye anatarajia kustaafu mwishoni mwa msimu huu. (Sky Sports)

Jean Michael Seri
Manchester United ilifuatilia mkataba wa kiungo wa klabu ya Nice, Jean Michael Seri wiki hii kwa lengo la kutaka kumsajili kwenye majira ya joto.

Arsene Wenger amemtaja kiungo anayekadiriwa kuwa na thamani ya ya pauni milioni 45 toka klabu ya Lyon, Nabil Fekir kuwa chaguo lake la kwanza kwenye usajili wa majira ya joto.

Arsenal ina uhakika wa kufanikisha uhamisho wa beki wa klabu ya West Brom, Jonny Evans kwa pauni milioni 25 mwishoni mwa msimu huu.

Jose Mourinho alifanya mazungumzo na Paul Pogba kwa muda wa saa moja katika ofisi zilizopo kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester United wiki hii.

Mstakabali wa maisha yajayo ya Eliaquim Mangala katika klabu ya Everton uko shakani baada ya kupata majeraha ya goti yanayoweza kumweka nje kwa muda mrefu. (Daily Mail)

Arsenal inafanya mpango wa kuwasili Nabil Fekir toka klabu ya Lyon na Timo Werner wa RB Leipzig kwenye majira ya joto.

Meneja wa klabu ya Leicester City, Claud Puel anasistiza kuwa, sakata la Riyad Mahrez limeisha na kwa sasa nyota huyo anatazamia kutumikia klabu hiyo kwa nguvu zake zote.
 
Klabu ya Arsenal inatarajiwa kufanya ziara nchini Uganda mwezi June mwaka 2019. (ESPN)

Kieron Dyer anasema kuwa inawezekana kitendo cha ubaguzi alichofanyiwa kingebakia kuwa siri kama isingekuwa Joey Barton. (Telegraph)

Sandro Ramirez
Sandro Ramirez ameiambia Everton kuwa hataki kurejea katika klabu ya Sevilla alikokuwa kwa mkopo.

Fulham ina matumaini ya kumsajili moja kwa moja kiungo wa klabu Brighton, Oliver Norwood kwenye majira ya joto.

Klabu ya Crystal Palace itamuuza kwa bei pungufu kiungo wa klabu hiyo, Jordon Mutchn kwenye majira ya joto.

Leeds United inatarajiwa kutoa ofa ya pauni milioni 4.5 kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Carpi, Jerry Mbakogu. (Mirror)

Arsenal imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig na Timu ya Taifa ya Ujerumani, Timo Werner anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 50.

Mchezaji aliyevunja rekodi ya usajili ya klabu ya Brighton kwa kusajiliwa kwa kiasi cha pauni milioni 14, Jurgen Locadia ni msanii maarufu nje ya uwanja anayetesa kwa nyimbo tatu kubwa hadi hivi sasa.

Timothy Fosu-Mensah
Manchester United inaaweza isitumie fedha nyingi kwenye usajili wa wachezaji wakati wa majira ya joto kutokana na kiwango ambacho Timothy Fosu-Mensah amekionyesha akiwa Crystal Palace kwa mkopo hadi hivi sasa. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 17 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 17 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/17/2018 11:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.