Loading...

Wapiga kura wakataa kuhalalisha bangi Ohio

BangiWatetezi wa kuhalalishwa kwa bangi walitumia mamilioni kwenye kampeni

Wapiga kura katika jimbo la Ohio, nchini Marekani wamekataa pendekezo la kuhalalisha matumizi ya bangi.

Pendekezo hilo lililopewa jina Issue 3 lingefanyia marekebisho sheria ya jimbo la Ohio na kuifanya kuwa halali kwa raia yeyote aliye na umri wa miaka 21, na zaidi, kutumia bangi kwa sababu za kibinafsi na za kimatibabu.
Kuhalalishwa kwa bangi kungewezesha bidhaa zilizotiwa bangi, kama vile peremende kuuzwa madukani. Raia wa kawaida pia wangeruhusiwa kukuza hadi mimea minne ya bangi.
Lakini kwa mujibu wa makadirio ya kura yaliyofanywa na vyombo vya habari humo, pendekezo hilo limeshindwa na kiwango cha kura cha mbili kwa moja.
Makundi yaliyotetea kuhalalishwa kwa bangi yalitumia hadi $12m kwenye matangazo kabla ya kura hiyo kupigwa Jumanne.
Sheria ya Issue 3 ingetoa idhini kwa bangi kukuzwa katika maeneo 10 jimbo la Ohio, jambo ambalo wakosoaji wanasema lingepelekea kuwepo kwa ukiritimba.
Kambi ya waliotetea sheria hiyo ilikuwa na watu mashuhuri wakiwemo msanii Nick Lachey, na Woody Taft, ambaye ni jamaa wa rais wa zamani wa Marekani William Howard Taft.
BangiBaadhi ya waliopinga waliogopa kungezuka ukiritimba
Pendekezo hilo lilipingwa vikali na hospitali zinazoshughulikia watoto, baadhi ya mashirika ya kibiashara na wakulima.
Majimbo ya Colorado, Washington, Oregon na Alaska, pamoja District of Columbia, yamehalalisha matumizi ya bangi kwa sababu za kujiburudisha.
Majimbo 20 nayo huruhusu matumizi ya bangi kwa sababu za kimatibabu.

Source: BBC
Wapiga kura wakataa kuhalalisha bangi Ohio Wapiga kura wakataa kuhalalisha bangi Ohio Reviewed by Zero Degree on 11/04/2015 10:49:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.