Utapeli mpya wa nyumba za mnada, ..wanunuzi wapewa tahadhari.
KAA chonjo, ukizubaa kidogo tu umetapeliwa. Hiyo ndiyo tahadhari muhimu wanayopaswa kuizingatia wale wote walioweka dhamana nyumba zao ili kujipatia mikopo kwenye taasisi mbalimbali za fedha.
Akielezea zaidi, Kuhanda alisema nyumba hiyo imerejeshwa baada ya kuuzwa katika mazingira ya utata na taasisi moja ya fedha mkoani Kilimanjaro kwa Sh. milioni 40, kupitia mnada hewa kwa madai ya kufidia deni linalotokana na mkopo wa Sh. milioni 45.
Alisema mkopo huo ulitumika kuweka rehani nyumba hiyo ambayo thamani halisi ya kitaalamu, iliyozingatia pia thamani ya ardhi katika eneo husika, ikiwa ni Sh. milioni 220.
Kuhanda alisema kuwa hadi mmiliki wa nyumba hiyo akishindwa kulipa deni husika, thamani ya mkopo ilikuwa imefikia Sh. milioni 65.
Alisema kilichoashiria utata ni nyumba hiyo kuuzwa kwa Sh. milioni 40, bei ambayo haifikii hata robo ya thamani yake halisi.
Alisema ofisi yake baada ya kuletewa suala hilo na kukamilisha uchunguzi wake, ilibaini kuwa nyaraka zilizotumika kuombea mkopo zilikuwa ni za kughushi na kwamba, hata kiapo cha mwenza kuridhia nyumba hiyo kuwekwa rehani kwa mkopo husika kilikuwa kimegushiwa.
Aidha, alisema taratibu za kuhakiki uhalali wa mkopo huo ziligubikwa na rushwa na hapakuwa na mnada ulioratibiwa.
Pia kazi ya kumtoa mwenye nyumba iliyofanyika Oktoba 22, mwaka huu na kuondosha vitu vyake kwa nguvu liliendeshwa kibabe kiasi cha kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na upotevu wa baadhi ya vitu.
Kasoro nyingine, kwa mujibu wa uchunguzi wa Takukuru, ni kampuni ya udalali inayodaiwa kuendesha mauzo ya nyumba hiyo uhalali wake pia unatia shaka.
Kuhanda aliwataka mawakili na wanasheria kutumia mihuri yao kutenda haki na siyo kuchangia kuwanyima wanyonge haki na pia kuwataka maofisa mikopo wa benki katika mkoa wao wa Kilimanjaro kuzingatia uadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa katika utoaji wa mikopo.
Aidha, tahadhari hiyo inafaa kuwakuta pia wanunuzi wa nyumba na mali zingine zinazowekwa dhamana ili kuhakikisha kuwa wanajiweka mbali na ‘dili’ za kitapeli zinazoweza kuwaweka pabaya na pia kupoteza fedha zao bila kutarajia.
Tahadhari kuhusiana na yote hayo imetolewa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kilimanjaro, Alex Kuhanda, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuokoa nyumba ya mkazi mmoja wa mji huo, iliyouzwa kiujanja kwa namna ya kumwongezea umasikini mmiliki wake huku mpango huo ukiwanufaisha wachache walioshiriki kuusuka.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kuhanda alisema tukio hilo lenye harufu ya rushwa hivyo kuwalazimu kuingilia kati kabla ya kuokoa mali ya raia asiye na hatia, lilitokea hivi karibuni na kuhusisha uuzaji ‘bandia’ kwa mnada wa nyumba hiyo yenye thamani ya Sh. milioni 220, lakini ikapigwa bei na wajanja kwa Sh. milioni 40 tu.
Nyumba hiyo ya familia, na ambayo sasa mmiliki wake amerejeshewa baada ya kuokolewa na Takukuru, iko katika eneo la Msaranga, Manispaa ya Moshi.
Kuhanda alisema wao wamefurahi kuona jitihada walizofanya zimefanikisha kuokolewa kwa nyumba hiyo, lakini akawataka wananchi wengine kuwa macho.
“Furaha yetu kama Takukuru ni kuona tumefanikiwa kusimamia urejeshwaji wa nyumba iliyokuwa imeuzwa kwa njia ya rushwa na nyaraka za kughushi. Tunafurahi kuona mama huyu (mmiliki aliyehifadhiwa jina) na watoto wake watasherehekea Krismasi na Mwaka Mpya wakiwa katika nyumba yao,” alisema Kuhanda.
Kwa mujibu wa Kuhanda, katika hali ya kawaida, nyumba hiyo ilikuwa vigumu kurejeshwa na kwamba kutokana na tukio hilo, sasa Takukuru inajipanga kupitia nyaraka zote zinazohusiana na mikopo katika benki zilizoko katika mkoa wa Kilimanjaro pamoja na madalali wa mahakama walivyosimamia haki katika mali mbalimbali zilizouzwa.
Taratibu nyingine za kisheria kuhusiana na uchunguzi uliowezesha kuokolewa kwa nyumba hiyo iliyookolewa na Takukuru zingali zikiendelea kuchukuliwa.
SAKATA LENYEWE

Source: Nipashe
ZeroDegree.
Utapeli mpya wa nyumba za mnada, ..wanunuzi wapewa tahadhari.
Reviewed by Zero Degree
on
12/24/2016 01:20:00 PM
Rating: