Viongozi wa upinzani na serikali nchini DRC wapata mwafaka wa mgogoro wao.
- 20 wauawa katika maandamano ya Kumpinga Rais Kabila nchini Congo.
- Rais Kabila atangaza kutogombea Urais tena katika uchaguzi mkuu ujao.
Viongozi wa Upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanasema kuwa muafaka umeafikiwa na chama tawala kuhusiana na ubadilishanaji wa mamlaka.
Katika makubaliano yaliyoongozwa na Kanisa Katoliki, Rais Joseph Kabila atasalia mamlakani hadi mwisho wa mwaka ujao wa 2017, licha ya muhula wake kumalizika rasmi.
Waziri mkuu mpya atachaguliwa kutoka mrengo wa upinzani, na muafaka huo utaalindwa na kinara mkuu wa upinzani, Etienne Tshi-sekedi.
Waziri mkuu mpya atachaguliwa kutoka mrengo wa upinzani, na muafaka huo utaalindwa na kinara mkuu wa upinzani, Etienne Tshi-sekedi.
- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika 'hatari kubwa'.
- Kabila kuongoza hadi 2017, ..ni baada ya Uchaguzi wa Rais nchini Congo kuahirishwa.
Bwana Kabila amehudumu kwa mihula miwili sawa na katiba ya taifa hilo, lakini uchaguzi mkuu umecheleweshwa.
Bwana Kabila amekataa kuachia madaraka hatua iliyosababisha maandamano mabaya katika barabara za miji ya taifa hilo.
Serikali imekubaliana na mapatano hayo ambayo upinzani inasema kuwa yatatiwa saini hatimaye leo Ijumaa.

ZeroDegree.
Viongozi wa upinzani na serikali nchini DRC wapata mwafaka wa mgogoro wao.
Reviewed by Zero Degree
on
12/24/2016 10:55:00 AM
Rating: