10 wanaoongoza kwa pasi nyingi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza [EPL]
Kiungo Paul Pogba huenda akachukua muda kumudu nafasi yake ya kuwa moja wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Manchester United.
Tayari takwimu zimeanza kuonyesha kuwa uwezo wake wa kupiga pasi umeweka rekodi mpya katika soka la England.
Mfaransa huyo amekuwa mchezaji wa kwanza kupiga pasi zaidi ya 1,000 akiwa kwenye nusu ya wapinzani wake hadi sasa katika msimu huu.
Takwimu hizo zinaonyesha Pogba amewafunika viungo wenzake kutoka Liverpool, Arsenal, Manchester City, Chelsea na Tottenham timu ambazo zinasifika kucheza soka la pasi nyingi kuliko Manchester United ya Jose Mourinho.
Pogba amepiga pasi 1,029 akiwa nusu ya wapinzani wake ikiwa ni pasi 42 zaidi ya kiungo wa Liverpool, Jordan Henderson aliyepiga pasi 987.
Mafanikio ya kiungo huyo mwenye miaka 23, yamewashangaza wengi na kuwaweka Man United katika nafasi nzuri wakiwa nyuma kwa mchezo moja kwa wapinzani wake katika mbio za kusaka ubingwa wa England.
Pogba aliweka rekodi hiyo wakati Man United ikishinda 2-0 dhidi ya Watford kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Takwimu zilizotolewa na EA Sports, mbali ya Pogba na Henderson wanaofuatia katika nafasi ya tatu ni kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil akipiga pasi 954 na kiungo wa Man City, David Silva anashika nafasi ya nne.
10 wanaoongoza kwa pasi nyingi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza [EPL]
Reviewed by Zero Degree
on
3/02/2017 10:28:00 AM
Rating: